Popular posts from this blog
GURUMO AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA NA WAZIRI KIKWETE
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Na Omary Mngindo, Kimange DIWANI wa Kata ya Kimange Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Pwani Juma Gurumo, amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu na Mbunge Ridhiwani Kikwete kwa kuiangalia kwa jicho la kipekee. Gurumo ametoa kauli hiyo Sept 17 akipokea mabomba yanayolenga kuboresha upatikanaji wa Maji, kutoka kutoka kwa Ofisa wa DAWASA Mhandis Kahemele, ambapo alisema Serikali imeonesha namna gani inavyowajali wanaKimange. "Nielezee shukrani zangu kwa Serikali yangu inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu pamoja na Waziri wa Utumishi Ridhiwani Kikwete ambae ndio Mbunge wangu, Kimange inakwenda kwa kasi kubwa," alisema Gurumo. Aliongeza kuwa ameingia kwenye nafasi hiyo akiwa mwenye bahati kubwa, kwani tangu achaguliwe mwaka mmoja uliopita kumekuwepo na kasi kubwa ya maendeleo yanayoelekezwa katani kwake. "Nimeingia na bahati kwani kwa kipindi kifupi tangu nichaguliwe kuwa Diwani Maji yanazidi kuongezewa miundombinu, sasa yanapatikana maeneo mengi na leo tunapokea mabom...
RAIS WA ZANZIBAR ATOA POLE KUFUATIA KIFO CHA MAMA FATMA KARUME.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa salamu za pole kwa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Amani Abeid Karume, pamoja na familia, ndugu na jamaa, kufuatia kifo cha Mama Fatma Karume, aliyekuwa mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, kilichotokea leo, tarehe 21 Septemba 2026. Rais Dkt. Mwinyi amesema amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa, akieleza kuwa anaungana na familia ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki cha majonzi. Amesema Marehemu Mama Fatma Karume amekuwa sehemu muhimu ya historia ya Zanzibar na Tanzania, akiwa mwenza wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar. Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu amsamehe na amrehemu Marehemu Mama Fatma Karume na amjaalie makaazi mema Peponi, pamoja na kuipa familia subira katika kipindi hiki kigumu.
JANETH MASABURI ATEULIWA KUWA MBUNGE.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
GREEN ACRES YAANZA KUFUNDISHA AKILI MNEMBA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
GREEN ACRES YAANZA KUFUNDISHA AKILI MNEMBA Na Mwandishi Wetu Mkururugenzi wa shule ya Green Acres ya Mbezi Beach Salasala jijini Dar es Salaam, Jacklline Rushaigo ameelezea namna shule hiyo ilivyoanza kufundisha Teknojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA ili kwenda sanjari na ulimwengu kidijitali. Akizungumza kwenye mahafali ya darasa la saba na shule ya awali ambapo wanafunzi 60 walihitimu elimu ya msingi, Jackline alisema Shule hiyo inatambua umuhimu wa kuzingatia teknolojia za kisasa katika ufundishaji. “Tumeongeza ubora na ufanisi kwenye TEHAMA, wanafunzi wetu wanajifunaza masuala ya akili mnemba wakiwa wadogo hapa shuleni na mambo yanayoendana na uhalisia wa utanzania wetu na dunia ya sasa,” alisema “Tunawapa taaluma ambayo hata wakiwa nje ya shule wanaweza kufanya vitu mbalimbali vya kujiajiri na kujiingzia kipato, Green Acres tunataka mwanafunzi akimaliza hapa awe na ujuzi wa kutosha kabisa kumwezesha kufanya mambo makubwa,” alisema Aliwataka wahitimu wa darasa l...
MWANRI AWAPA SOMO MAKADA WALIONOLEWA.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MWANRI AWAPA SOMO MAKADA WALIONOLEWA. Na Omary Mngindo, Kibaha NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Aggrey Mwanri amewataka washiriki wa Mafunzo ya Makada wa vyama vya kisiasa kwenda kuyatumia vizuri. Mwanri ametoa Rai hiyo katika kufunga Mafunzo ya siku 45 ya uongozi kwenye shule ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoa wa Pwani, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Msumbiji (FRELIMO), Chakil Aboobacar. "Mafunzo haya yanaashiria mwanzo wa kukiandaa kizazi kijacho cha Makada na viongozi wa vyama dada kutoka nchi zetu, niwaombe mkawe mabalozi wazuri wa kuyaeleza mliyojifunza," alisema Mwanri. Alipongeza kuwa, "Mmepata nafasi ya kujifunza masuala yanayohusu maendeleo ya nchi zetu, Wakufunzi wamenyakai kubwa sasa ni wajibu wenu kwenda kwenye vyama vyeu mkaunganishe vyama vyenu, Serikali na Wananchi,"alisema Naibu Katibu huyo. Mkuu wa Shule hiyo Prof. Marcelina Chijoriga alisema kuwa mafunzo yalitaraji kuwa na washiriki 60 ikiwa ni walengwa ...
WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
NA HADIJA OMARY, LINDI. Wazee wa Nachingwea wameaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba mwaka huu 2024. Wito huo umetolewa na Afisa Uchaguzi wa Wilaya ya Nachingwea Robert Mmari alipokuwa akizungumza na wazee maarufu wa Wilaya hiyo ambapo amesisitiza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na msaada wa wazee utahakikisha zoezi linafanikiwa Afisa Uchaguzi (W) ya Nachingwea ndugu Robert Mmari pia ameeleza kuwa sifa za mgombea na mpiga kura zimesha ainishwa, kwamba Mpiga kura lazima awe na akili timamu, awe na umri wa miaka 18 au zaidi, na awe mkazi wa kitongoji husika Wananchi wote wanatakiwa kupiga kura kwenye vitongoji walivyojiandikisha, huku zoezi la kuchukua fomu za kugombea likipangwa kuanza Novemba 1 Aidha, Msaidizi wa uchaguzi Joshua mnyang'ali Amesema kuwa kwa mwananchi kushindwa kujiandikisha kwa wakati uliopangwa, atapoteza h...
MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA ZAIDI YA BIL 4 IGUNGA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA ZAIDI YA BIL 4 IGUNGA Na Allan Kitwe, Igunga MIRADI ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 4.8 Wilayani Igunga Mkoani Tabora imekaguliwa, kuwekewa jiwe la msingi na kuzinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda. Akiongea na wananchi katika maeneo mbalimbali ambako mwenge huo umepita Kiongozi huyo ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mabilioni ya fedha katika Wilaya hiyo. Amesisitiza kuwa Mwenge wa Uhuru Kitaifa umeridhika na kazi iliyofanyika kwenye utekelezaji miradi ya wananchi ndio maana ameweka jiwe la msingi na kuzindua miradi yote kwa sababu imejengwa kwa ubora unaotakiwa. ‘Nakupongeza sana Mkuu wa Wilaya Sauda Mtondoo, Mkurugenzi Mtendaji Selwa Hamid na Wataalamu wote kwa kusimamia vizuri na kwa dhati fedha zilizoletwa kwa ajili ya kutekeleza miradi hii’, ameeleza. Miradi iliyotembelewa na kuzinduliwa na Kiongozi huyo ni mrad...
MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi (darasa la saba) kwa mwaka 2018 ambapo matokeo yanaonyesha ongezeko la ufaulu kwa asilimia 4.76% tofauti na ufaulu wa 2017 ambao ulikuwa asilimia 72.76%. Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Dkt. Charles Msonde, amesema katika tathmini ya awali kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 4.9% ikilinganishwa na 2017, amesema pia kiwango cha ufaulu wa somo la Kiingereza uko chini sana tofauti na masomo mengine (50%). NECTA pia limewafutia matokeo watahiniwa 357 waliobainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani iliyofanyika mwaka huu 2018. “Baraza limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa zaidi 100 kutokana na kuugua kipindi cha mtihani na kuwapa fursa ya kufanya mtihani huo mwaka 2019,” amesema Msonde. Bonyeza link hapo chini kuona matokeo ya kila shule. NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2018 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR...
TITF YAANDAA TAMASHA LA SANAA ZA UFUNDI ARUSHA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
TITF YAANDAA TAMASHA LA SANAA ZA UFUNDI ARUSHA Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Tanzania International Tourism Festival (TITF) imeandaa tamasha la Sanaa za ufundi litalalofanyika kuanzia tarehe 6 hadi 11 Oktoba jijini Arusha. Tamasha hilo linalenga kuunganisha Sanaa, Ufundi, Utamaduni, Utalii na Uchumi wa Ubunifu, pamoja na kutoa fursa za masoko, biashara na uwekezaji kwa wazalishaji wa bidhaa za Sanaa na ufundi. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Edward Buganga alisema TITF imezishirikisha BASATA, Bodi ya Filamu Tanzania na COSOTA katika maeneo yanayohusiana na majukumu yao. Alisema tamasha hilo litafanyika katika Viwanja vya General Tyre, Njiro, Arusha. Alisema BASATA itashiriki katika maeneo yanayohusu maendeleo na ukuzaji wa sanaa, wasanii na wadau wa sanaa, pamoja na kuhamasisha fursa zinazotokana na uchumi wa ubunifu. Buganga alisema Bodi ya Filamu Tanzania itashiriki katika maeneo yanayohusu tasnia ya filamu na ...


Comments
Post a Comment