STAMICO PELEKENI UJUZI WENU MASHIRIKA MENGINE- BALILE.

 

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ameshauri Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kupeleka ujuzi wake katika mashirika mengine ya serikali kutokana na mafanikio yake.


Balile alitoa kauli hiyo leo tarehe 28 Agosti 2023, jijini Dar es Salaam wakati STAMICO lilipokutana na wahariri kuelezea safari ya shirika hilo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972.


Awali, Mkurugenzi Mrendaji wa shrika hilo Dk. Vanance Mwasse alisema, katika miaka mitatu nyuma shirika hilo lilikuwa likizalisha jumla ya Tsh 1.3 Bilioni kwa mwaka, lakini lilikuwa likipata ruzuku Tsh. 3.4 Bilioni kila mwaka kwamba, lilikuwa likizalisha hasara.


Amesema, sasa shirika hilo linazalisha Tsh. 61.1 Bilioni kwa mwaka akisisitiza mafanikio hayo yametokana na wafanyakazi wote kubadilika na kuweka mipango na kisha kuitekeleza.


“Mafanikio hayaji tu. Tumeamua kubadilika, tumekuwa tukipanga na kuhakikisha tunatekeleza kile tulichokipanga ndio maana tumefika hapa,” amesema.






 

Comments

Popular posts from this blog

GURUMO AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA NA WAZIRI KIKWETE

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

RAIS WA ZANZIBAR ATOA POLE KUFUATIA KIFO CHA MAMA FATMA KARUME.

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

GREEN ACRES YAANZA KUFUNDISHA AKILI MNEMBA

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA ZAIDI YA BIL 4 IGUNGA

MWANRI AWAPA SOMO MAKADA WALIONOLEWA.