Thursday, August 17, 2023

VIONGOZI WA WIZARA YA UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO WAENDELEA KUPATA UZOEFU WA MAGEUZI YA UTENDAJI

 


Na Shamimu Nyaki


 Viongozi na Wakuu wa Taasisi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wameendelea kupokea elimu kupitia Mada mbalimbali zinazotolewa na viongozi na Wataalam mbalimbali katika nyanja tofauti katika Kikao cha Faragha cha siku tatu cha viongozi hao kinachoendelea leo Agosti 17, 2023 mkoani Morogoro.


Viongozi hao chini ya Mwenyekiti, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu wamepokea Mada kuhusu Itifaki na Ustaarabu iliyowasilishwa na Bw. Batholomeo Jungu, Mkurugenzi wa Maadhimisho kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Mada kuhusu Rasilimaliwatu kama dhamana ya Taasisi iliyowasilishwa na Bw. David Nchimbi kutoka Taasisi ya Deloitte and Touche.


Maada nyingine ni Mabadiliko ya Kitaasisi kupitia uzoefu wa NSSF iliyowasilishwa na Mhe. Balozi Dkt. Ramadhan Kitwana Dau pamoja na Mada ya Tatizo letu ni nini dhidi ya matarajio yetu iliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu.


Aidha, Viongozi hao pia walipokea Mada kuhusu Sifa ya Uongozi katika ulimwengu wa kisiasa iliyowasilishwa na Bw. Kadari Singo kutoka Uongozi Institute ambapo walipata nafasi ya kuzijadili, kuuliza maswali, kutoa maoni, ushauri na kupata ufafanuzi wa maswala mbalimbali. 












No comments:

Post a Comment