MWANRI AWAPA SOMO MAKADA WALIONOLEWA.

 

MWANRI AWAPA SOMO MAKADA WALIONOLEWA.


Na Omary Mngindo, Kibaha



NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Aggrey Mwanri amewataka washiriki wa Mafunzo ya Makada wa vyama vya kisiasa kwenda kuyatumia vizuri.


Mwanri ametoa Rai hiyo katika kufunga Mafunzo ya siku 45 ya uongozi kwenye shule ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoa wa Pwani, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Msumbiji (FRELIMO), Chakil Aboobacar.


"Mafunzo haya yanaashiria mwanzo wa kukiandaa kizazi kijacho cha Makada na viongozi wa vyama dada kutoka nchi zetu, niwaombe mkawe mabalozi wazuri wa kuyaeleza mliyojifunza," alisema Mwanri.


Alipongeza kuwa, "Mmepata nafasi ya kujifunza masuala yanayohusu maendeleo ya nchi zetu, Wakufunzi wamenyakai kubwa sasa ni wajibu wenu kwenda kwenye vyama vyeu mkaunganishe vyama vyenu, Serikali na Wananchi,"alisema Naibu Katibu huyo.


Mkuu wa Shule hiyo Prof. Marcelina Chijoriga alisema kuwa mafunzo yalitaraji kuwa na washiriki 60 ikiwa ni walengwa 10 kutoka kila chama, lakini wemehudhuria 37 ambao ndio wamehitimu.


"Tulikuwa na Wataalamu wazuri ambao wamewanoa Vijana wetu ambao leo wanaitimu Mafunzo yao ya siku 45, pia wamo baadhi ya Mawaziri waliopita, Makatibu Wakuu Wastaafu, Maprofesa na Wakufunzi mbalimbali wenye sifa za juu," alisema Chijoriga.


Kwa upande wake Mgeni rasmi Katibu wa Frelimo Aboobacar, amewataka wataalamu kutoka vyama vya ukombozi waliomaliza mafunzo hayo ya Ukuzaji wa Wakufunzi (ToT) kutumia maarifa waliyoyapata kuviwezesha vyama vyao.


"Hii ni kozi itayoleta mwanga mpya hasa katika kipindi hiki tunachoshuhudia changamoto miongoni mwa jamii zetu, tunatakiwa kwenda kutumia fursa hii kutokukubali kugawanywa, badala yake tukanyekazi kwa bidii na kwa umoja," alisema Abobaca.


Akizungumza na Waandishi baada ya hafla hiyo, Prof. Elisante Ole Gabriel alisema kuwa mafunzo hayo yamekuwa na mafanikio, na kwamba ana uhakika kwamba yanakwenda kufanyiwakazi.


Katika hafla hiyo pia imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, wajumbe kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mabalozi na Makamishna Wakuu, watafiti, wanafunzi wa vyuo vikuu, wasomi na taasisi binafsi.


Comments

Popular posts from this blog

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.

KIKWETE AITAKA TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAKULA NA UCHUMI WA BULUU