Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete ameendelea na ziara ya Mkoa wa Singida kwa kutembelea Wilaya ya Manyoni na mtaa wa Ughaugha katika manispaa ya Singida kukagua na kuongea na wananchi wanaofaidika na miradi ya kunusuru kaya zilizo kwenye umaskini mkubwa zinazosaidiwa na mradi wa TASAF.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara hiyo ya siku mbili, Naibu Waziri Kikwete amewaomba viongozi katika ngazi zote hasa Halmaashauri , kuunga mkono hatua kubwa zinazofanywa na Mradi wa TASAF kuwaondoa wananchi katika hali mbaya za kiuchumi na kuwaunganisha na fursa mbalimbali zilizopo nchini hasa zile zinazotolewa na Halmashauri zetu.
Akizungumza mbele ya wananchi , alieleza kuwa miradi ya TASAF ni miradi ambayo imepangwa vizuri na hata usimamizi wake ni mzuri na ndiyo maana matokeo yanaonekana.
Naibu Waziri Kikwete amemaliza ziara hiyo ya siku mbili kwa kuendelea kuwaomba wananchi waendelee kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi nzuri na kubwa anayoifanya.
No comments:
Post a Comment