Akizungumza na Watumishi waliojaa kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, Naibu Waziri wa Utumishi, Ridhiwani Kikwete, aliwakumbusha hatua mbalimbali zilizofanywa na serikali kutatua kero mbalimbali za watumishi ikiwemo kero ya kutopanda madaraja kwa muda mrefu, madai ya malimbikizo ya madeni na mishahara na kupanda vyeo na maslahi mengineyo.
Akizungumzia mbele ya Watumishi hap amewaambia kuwa katika mwaka uliokwisha wafanyakazi zaidi ya 454,508 wamepandishwa madaraja, watumishi 101,651 wamebadilishiwa mishahara kutumia mfumo wa HCMIS, watumishi 4454 wamebadilishiwa Muundo, 126,924 kati ya waliokuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara walilipwa na ajira mpya 43,646 zilitolewa.
Na kwa takwimu hizo pia Watumishi wa kada mbalimbali wa Halmashauri hiyo walifaidika.
Naibu Waziri aliwahakikishia Viongozi wa Halmashauri hiyo pia, serikali itaendelea kupunguza mapungufu ya Ikama ya wafanyakazi kadri utekeleza wa mipango ya kibajeti inavyoendelea kutekelezwa na hasa baada ya kupatiwa watumishi zaidi ya 227 Katika bajeti iliyopita ya 2022/2023.
Pamoja hayo Naibu Waziri aliwahakikishia watumishi hapa kuwa serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania imeendelea kutengeneza mazingira wezeshi ya Watumishi kufanya kazi na kwamba serikali imeendelea kuweka mazingira na kuhakikisha kuwa mazingira mazuri ya kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment