Kamati ya Watalaamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imefanya ziara na kukagua ujenzi wa Shule ya Msingi Kiharaka na kuridhishwa na maendeleo yake.
Ujenzi huo unahusisha vyunba vya madarasa kumi na nne (14), jengo la Utawala, Ofisi za Walimu 6 na matundu 16 ya vyoo, pia vyumba viwili vya madarasa ya shule ya msingi Awali yanayojengwa kwa msaada wa mradi wa BOOST vinaendelea kujengwa.
Akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo Mhandisi wa Ujenzi Bw. Respicius Selestin amesema wameridhishwa na ujenzi huo, kwa namna unavyoendelea.
Aidha amemtaka mkandarasi anaefanya shughui hiyo kukamilisha maeneo ambayo hayajakamilka kwa haraka ili majengo hayo yaweze kutumika kikamilifu.
"Mafundi malizieni haya maeneo ambayo hayajakamilika kwa kufanya finishing na final touches, ili majengo haya yatumike " alisema Bw. selestin.
Akimuwakilisha Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Bagamoyo Bi. Madina Mussa alimuagiza Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kusimamia kwa umakini mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.
Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kiharaka Bw. john Angelo ameishukuru kamati kwa kutembelea na kujionea ujenzi wa mradi huo, huku akipokea maelekezo yote yaliyotolewa na kamati.
"Tumepokea maelekezo ya kamati tuna imani kwa kushirikiana na Mafundi mradi huu utakamilika haraka, mpaka kufikia tarehe 1 Septemba 2023 tutakuwa tumekamilisha ujenzi huu".
No comments:
Post a Comment