Monday, August 28, 2023

UFARANSA KUPIGA MARUFUKU VAZI LA ABAYA SHULENI.

 

Vazi la Abaya (Baibui) ambalo mara nyingi huvaliwa na wasichana wa dini ya kiislamu limepigwa marufuku nchini Ufaransa kuvaliwa shuleni.


Waziri wa Elimu wa nchi hiyo, Gabriel Attal amesema Mwanafunzi anapoingia darasani hatakiwi kutambuliwa kwa dini yake unapomuangalia.


Ufaransa pia imepiga marufuku alama kubwa za Kidini katika Shule na Majengo ya Serikali kwa maelezo zinakiuka Sheria ya Nchi hiyo.


Wizara ya Elimu imesema Kanuni hiyo inatarajiwa kuanza Mwaka mpya wa masomo wa Septemba 4, 2023 katika shule zote za Serikali nchini humo.



No comments:

Post a Comment