MOJA YA NDOTO YANGU KUHAKIKISHA MAFIA INAENDELEA KUWA SEHEMU DAIMA YA UPENDO AMANI NA MSHIKAMANO KWA KUMTANGULIZA MUNGU-QS KIPANGA"
MWANDISHI WETU
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia Mhe Qs Omar Kipanga ameongoza Mamia ya Waumini katika Maombi ya kuliombea taifa pamoja na viongozi mbalimbali wa Kitaifa katika Kuendelea kuwa na imani na Upendo kwa Jamii.
Akiziungumza wakati wa kongamano la amani na Upendo amesema miongoni mwa matarajio yake ni Kuendelea kuhakikisha kwamba Jimbo la Mafia linaendelea kuwa sehemu ya Upendo amani na mshikamano kwa watu wake Kila siku,
"Nafanya Kazi huku nawaza Kila siku kumuomba Mwenyezi mungu atubariki na kutuongoza katika Shughuli zetu za Kila Siku katika Amani, Upendo mshikamano kama ambavyo viongozi Wetu wanavyofanya kwa taifa letu hasa RAIS Dr Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dr Philip Mpango na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa alimalizia Mhe Qs Kipanga"
"Tumebahatika Tanzania kuwa na amani Upendo na Mshikamano basi tuendelee kuwaombea Dua Viongozi Wetu kwa Mwenyezi mungu kutuongoza Daima kwa Misingi ya Kumjua Mwenyezi mungu ili tubarikiwe katika mambo yetu sisi na Vizazi vyetu alisisitiza Mhe Qs Kipanga"
*"Kama unataka kuwa na amani ya Moyo kuwa na utamaduni wa Kusoma kitabu Cha Mwenyezi mungu Kila siku asubuhi na usiku wakati wa kulala utabarikiwa sana na Utakua na moyo wa Upendo kwa ndugu jamaa Zako lakini pia Utakua na Imani Ambayo itakuondosha na chuki na wivu alishauri Mhe Qs Kipanga Kipanga*"
No comments:
Post a Comment