Tuesday, August 15, 2023

SERIKALI YAWEKA KATAZO LA UWEKAJI WA MIFUKO LAINI KWENYE CHUPA ZA VINYWAJI

Mwandishi Wetu.

Serikali imepiga marufuku matumizi ya mirija ya plastiki na kuweka plastiki laini katika chupa za vinywaji vinavyozalishwa nchini na zinazoingizwa kutoka nje ya nchi,

Akizungumza na Waandishi wa habari katika Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,( Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amesema Serikali inaelekeza wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa hizo kwa kuzingatia umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

*"Tunatoa muda baada ya muda huo basi hatutarajii kuona bidhaa zinazalishwa zikiwa na ile karatasi laini kwenye kifuniko". Amesema Waziri Jafo.*

Amesema baada ya miezi sita kumalizika wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa wanaelekezwa kuzalisha bidhaa zao bila kuweka plastiki laini nje ya chupa za vinywaji.

*"Bidhaa zinazozalishwa na kuingia sokoni kabla ya katazo hili ambazo muda wake wa mwisho wa matumizi haujafika zitaendelea kubaki sokoni hadi pale muda wake wa matumizi utakapokamilika". Amesema.*

Aidha amesema bidhaa zitakazozalishwa baada ya miezi sita kuanzia tarehe ya katazo hazitaruhusiwa kuingia sokoni.

Pamoja na hayo ameelekeza hoteli, migawaha na maduka ya vinywaji kutotumia mirija ya plastiki kwa kunywea vinywaji baada ya miezi sita kwani mirija hiyo imekuwa inaleta uchafuzi wa mazingira.

"Tunatarajia baada ya miezi sita watu watumie mirija mbadala kuliko kutumia mirija ya plastiki ambayo inafanya uchafuzi mkubwa wa mazingira".Amesema Waziri Jafo.





 

No comments:

Post a Comment