Popular posts from this blog
DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka, leo ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Kodi ya Wilaya kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Kikao hicho kimejadili tathmini ya mwenendo wa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na kuweka mikakati ya kuimarisha makusanyo kwa mwaka 2026/2027. Akizungumza katika kikao hicho, Shaka amesema kazi ya kukusanya kodi sio ukusanyaji tu, bali ni ujenzi wa maendeleo. "Sisi sio wakusanya kodi tu, bali ni wajenzi wa maendeleo. Kila shilingi tunayokusanya kwa haki na uadilifu, tunajenga kesho bora ya wananchi wetu. Hivyo jukumu letu sio dogo," alisema Shaka. Aidha, Shaka ameelekeza kila chanzo cha mapato Wilayani humo kipitiwe upya. "Kile ambacho kimekufa kifufuliwe, kile ambacho kinalala kiamshwe. Lazima tubadili mtazamo kutoka kudhibiti kwenda kuelimisha umma," alisisitiza. Ameitaka TRA na Halmashauri kuimarisha matumizi ya takwimu halisi (Da...
SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA Na Allan Kitwe, Tabora JUMLA ya silaha za moto 17 na risasi 19 zimesalimishwa kwa hiari katika Vituo vya Polisi na Ofisi za Serikali za Vijiji na Kata Mkoani Tabora kufuatia zoezi linaloendelea nchi nzima la usalimishaji silaha haramu kwa hiari bila kushtakiwa. Hayo yamebainishwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Twaha Lulengelule, alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa zoezi hilo limeanza Septemba 1, 2026 na litamalizika Oktoba 31, 2026. Amefafanua kuwa zoezi hilo linaloendeshwa na Jeshi la Polisi nchi nzima limelenga kuhakikisha silaha haramu zote zikiwemo zile zinazomilikiwa na watu au taasisi kinyume na taratibu zinasalimishwa kwa hiari kwa msamaha pasipo kushtakiwa. ‘Zoezi hili ni muhimu sana, naendelea kutoa wito kwa wananchi kutekeleza kwa hiari kabla ya kipindi cha msamaha wa kutokushtakiwa kumalizika ifikapo Oktoba 31, 2026 kinyume na hapo mkondo wa sheria utachukua...
NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MAKAMU WA RAIS MHE. NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE, KERO ZA WANANCHI ZITATULIWE Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Halmashauri zake kuhakikisha hali ya Dampo la Pugu inaboreshwa, huku akielekeza maeneo ya makazi yanayozunguka dampo hilo kupuliziwa dawa ili kuwalinda wananchi dhidi ya wadudu na kupunguza hatari ya magonjwa, hususan katika kipindi cha mvua. Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo leo, Septemba 18, 2026, alipofanya ziara katika Dampo la Pugu linalotumika kukusanya taka za Mkoa wa Dar es Salaam ili kujionea hali halisi ya eneo hilo na kusikiliza kero za wananchi wanaoishi maeneo ya jirani. Aidha, ameelekeza kuandaliwa kwa mpango kazi wa pamoja utakaoainisha hatua za haraka na za muda mrefu za kukabiliana na changamoto za uendeshaji wa Dampo la Pugu pamoja na kero zinazowakabili wananchi wanaoishi katika maeneo yanayolizunguka, ikiwemo kutopuliziwa dawa ...
GURUMO AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA NA WAZIRI KIKWETE
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Na Omary Mngindo, Kimange DIWANI wa Kata ya Kimange Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Pwani Juma Gurumo, amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu na Mbunge Ridhiwani Kikwete kwa kuiangalia kwa jicho la kipekee. Gurumo ametoa kauli hiyo Sept 17 akipokea mabomba yanayolenga kuboresha upatikanaji wa Maji, kutoka kutoka kwa Ofisa wa DAWASA Mhandis Kahemele, ambapo alisema Serikali imeonesha namna gani inavyowajali wanaKimange. "Nielezee shukrani zangu kwa Serikali yangu inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu pamoja na Waziri wa Utumishi Ridhiwani Kikwete ambae ndio Mbunge wangu, Kimange inakwenda kwa kasi kubwa," alisema Gurumo. Aliongeza kuwa ameingia kwenye nafasi hiyo akiwa mwenye bahati kubwa, kwani tangu achaguliwe mwaka mmoja uliopita kumekuwepo na kasi kubwa ya maendeleo yanayoelekezwa katani kwake. "Nimeingia na bahati kwani kwa kipindi kifupi tangu nichaguliwe kuwa Diwani Maji yanazidi kuongezewa miundombinu, sasa yanapatikana maeneo mengi na leo tunapokea mabom...
JANETH MASABURI ATEULIWA KUWA MBUNGE.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
TAKUKURU KAGERA YAOKOA ZAIDI YA BILIONI 2.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Na Alodia Babara, Bukoba. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imefanikisha uokoaji wa zaidi ya sh bilioni 2.7 kutoka kwa makampuni binafsi 146 yaliyokuwa wadaiwa sugu wa michango ya wafanyakazi wao katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kati ya jumla ya Sh5.2 bilioni zilizokuwa zinadaiwa. Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Kagera Ismail Bukuku akizungumza na waandiahi wa habari Septemba 16, 2026 amesema, hatua hiyo imechukuliwa baada ya ofisi yake kufuatilia madeni hayo na kuchukua hatua dhidi ya waajiri waliokuwa hawawasilishi kwa wakati fedha za michango ya wafanyakazi wao katika mfuko huo. "Waajiri hawa walishindwa kulipa michango ya wafanyakazi wao kwa kipindi cha miaka 9 kuanzia mwaka 2017 hadi Julai 2026 iliyofikia kiasi cha sh bilioni 5.2" amesema Bukuku Alieleza kuwa, oparasheni hiyo ilifanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza oparasheni ilianza Julai 22 hadi Agosti 5 huku awamu ya pili ...
MAGAZETI YA TANZANIA LEO TAREHE 16 SEPTEMBA 2026
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
RAIS WA ZANZIBAR ATOA POLE KUFUATIA KIFO CHA MAMA FATMA KARUME.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa salamu za pole kwa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Amani Abeid Karume, pamoja na familia, ndugu na jamaa, kufuatia kifo cha Mama Fatma Karume, aliyekuwa mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, kilichotokea leo, tarehe 21 Septemba 2026. Rais Dkt. Mwinyi amesema amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa, akieleza kuwa anaungana na familia ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki cha majonzi. Amesema Marehemu Mama Fatma Karume amekuwa sehemu muhimu ya historia ya Zanzibar na Tanzania, akiwa mwenza wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar. Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu amsamehe na amrehemu Marehemu Mama Fatma Karume na amjaalie makaazi mema Peponi, pamoja na kuipa familia subira katika kipindi hiki kigumu.
GREEN ACRES YAANZA KUFUNDISHA AKILI MNEMBA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
GREEN ACRES YAANZA KUFUNDISHA AKILI MNEMBA Na Mwandishi Wetu Mkururugenzi wa shule ya Green Acres ya Mbezi Beach Salasala jijini Dar es Salaam, Jacklline Rushaigo ameelezea namna shule hiyo ilivyoanza kufundisha Teknojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA ili kwenda sanjari na ulimwengu kidijitali. Akizungumza kwenye mahafali ya darasa la saba na shule ya awali ambapo wanafunzi 60 walihitimu elimu ya msingi, Jackline alisema Shule hiyo inatambua umuhimu wa kuzingatia teknolojia za kisasa katika ufundishaji. “Tumeongeza ubora na ufanisi kwenye TEHAMA, wanafunzi wetu wanajifunaza masuala ya akili mnemba wakiwa wadogo hapa shuleni na mambo yanayoendana na uhalisia wa utanzania wetu na dunia ya sasa,” alisema “Tunawapa taaluma ambayo hata wakiwa nje ya shule wanaweza kufanya vitu mbalimbali vya kujiajiri na kujiingzia kipato, Green Acres tunataka mwanafunzi akimaliza hapa awe na ujuzi wa kutosha kabisa kumwezesha kufanya mambo makubwa,” alisema Aliwataka wahitimu wa darasa l...


Comments
Post a Comment