Na Mwandishi Wetu, Dar
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limefanya mageuzi makubwa ambayo yameliwezesha shirika hilo kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni 1.3 hadi shilingi bilioni 61.1 sawa na ongezeko la asilimia 4425.
Hayo yamebainishwa leo Agosti 28,2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, CPA Dkt.Venance Mwasse katika kikao kazi kati ya shirika hilo na wahariri wa vyombo vya habari nchini, chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Amesema, mafanikio hayo yameliwezesha shirika sasa kuanza kutoa gawio serikalini, kwani tangu lianzishwe mwaka 1972 lilikuwa halijawahi kupeleka kitu chochote serikalin.
Dkt.Mwasse amefafanua kuwa, sababu zilizowawezesha kufikia mafanikio hayo ni kwa kubadili fikra,ushirikishwaji, nidhamu, kujiwekea malengo na kuyatekeleza
Kwa ujumla, tulifikia mahali ikabidi tubadilike kifikira, kuna mashirika ya umma ambayo yanayotoa huduma na kuna mashirika ya umma ambayo yanatakiwa yajiendesha kibiashara.
“Na mimi kama kiongozi kwa kulitambua hili ni shirika la umma nikaona lazima tuumize vichwa, pamoja na kuongeza morali ya wafanyakazi kwa kuona wanajaliwa na mipango iwe inanyooka.
"Pamoja na kuongeza nidhamu kwenye matumizi ya fedha za umma, na tuchague sehemu sahihi, kwa sababu sehemu za kuweka fedha ni nyingi, hivyo unaangalia penye faida.
Katika hatua nyingine, Dkt.Mwasse amesema, wanaendelea kuongeza uzalishaji wa mkaa mbadala ili kuondoa matumizi ya mkaa unaotokana na miti na matumizi ya kuni.
“Mikakati yetu ni kuendelea kuzalisha kwa wingi ili kuendelea kuwa kimbilio na tumani kwa watumiaji wengi nchini.
Mkataba huo ambao una thamani ya bilioni 55.2 na ulitiwa saini Machi 27,2023.
Dkt.Mwasse amesema, mkataba huo ni uthibitisho kuwa watanzania wanaweza kushiriki kikamilifu katika kandarasi zinatokea katika mnyororo wa thamani wa madini nchini.
“Tumeweka jicho letu la kipekee hapa, tutaendelea kuwapa mafunzo, na kubwa zaidi tutahakikisha benki ya wachimbaji inaanzishwa ili kuondoa changamoto ya wachimbaji, mpaka sasa hivi hakuna benki ya wachimbaji.
Kwa hiyo tunaamini pamoja na kuwaunganisha na benki mbalimbali, lakini tunaamini benki hii itakuwa mkombozi kwao.”
No comments:
Post a Comment