MKURUGENZI MTENDAJI BAGAMOYO ATEMBELEA MRADI WA KITUO CHA AFYA FUKAYOSI


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Bagamoyo, Mhe. Shauri Selenda Amefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya kilichopo katika kata ya Fukayosi.

Katika ziara hiyo Mkurugenzi huyo alitembelea majengo ya OPD, Maabara na Wodi zilizopo katika Kituo hicho, pia alikagua maendeleo ya utengenezaji wa miundombinu ya Maji taka na Umeme.

Aidha Mkurugenzi aliagiza kuharakishwa kwa ujenzi huo kwani wananchi wanasubiri huduma kutoka kwenye kituo hicho.

"Mganga Mfawidhi naomba ufuatilie suala la umeme na unipatie taarifa zote juu ya upatikanaji wa umeme hapa nakupa wiki moja suala hili liwe limekamilika, wananchi wanasubiri kituo hiki kikamilike ili waweze kupata na kufurahia huduma za Afya" Alisema Mkurugenzi.

Nae mganga mfawidhi wa Kituo cha Afya Fukayosi Dkt Ally akipokea maelekezo hayo aliahidi kufuatilia kazi zote ambazo hazijakamilika, ziweze kukamilika kwa wakati na hatimae Kituo hicho kianze kufanya kazi.








Comments

Popular posts from this blog

GURUMO AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA NA WAZIRI KIKWETE

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

RAIS WA ZANZIBAR ATOA POLE KUFUATIA KIFO CHA MAMA FATMA KARUME.

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

GREEN ACRES YAANZA KUFUNDISHA AKILI MNEMBA

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA ZAIDI YA BIL 4 IGUNGA

MWANRI AWAPA SOMO MAKADA WALIONOLEWA.