Monday, August 28, 2023

KARIM MANDONGA APIGWA NA OTHMANI KILUWA ZANZIBAR .

 

Bondia Karim Mandonga amepigwa kwa pointi na Othmani Kiluwa katika pambano la Tamasha la Uzinduzi wa Mchezo wa Ngumi Zanzibar 

Pambano hilo la Raundi Sita limeshuhudiwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ambaye amezindua mashindano hayo yaliyopigwa marufuku Kisiwani hapo zaidi ya mika 50 iliyopita ambapo Majaji wote watatu wamempa ushindi Kiluwa kwa pointi 55-56, 56-58 na 55-59

Hii ni mara ya tatu mfululizo Mandonga kupigwa. Julai 22 alipoteza pambano la marudiano na Mkenya Daniel Wanyonyi, na Julai 29 alipoteza pambano dhidi ya mganda Moses Golola

No comments:

Post a Comment