Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo
kushoto akipeana mkono wa pongezi na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha
kuchakata zao la muhogo mara baada ya halfa ya kuweka jiwe la msingi
katika kiwanda hicho amabcho kimejengwa katika kijiji cha Mgenge kata ya Beta
Wilayani Mkuranga.
.............................
VICTOR
MASANGU, MKURANGA
KILIO cha muda mrefu ambacho kilkuwa
kinawakabili wakulima wa zao la muhogo katika Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani
hatimaye hivi karibuni wanatarajia kuondokana na changamoto
sugu ya upatikanaji wa soko la uhakika kufuatia kuanza kwa
ujenzi wa mradi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata zao hilo
ambacho kitagharimu kiasi cha shilingi bilioni 9.5.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya
wakulima hao wakati wa Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo wakati wa halfa ya uwekeaji wa jiwe la msingi katika kiwanda
hicho ambacho kimejengwa na mwekezaji kutoka nchini China katika kijiji cha
Mkenge kata ya Beta Wilayani Mkuranga ambapo wamedai hapo awali walikuwa
na tatizo la kuuza mihogo yao kwa bei ya hasara.
“Sisi kama wakulima wa zao hili la
muhogo katika Wilayah hii ya Mkuranga tumefarijika sana kwa ujio wa mradi wa kiwanda
hiki ambacho kimejengwa na marafiki zetu wa kutoka nchini china, na tunashukuru
kwa jitihada ambazo zinafanywa na Mkuu wetu wa Mkoa wa Pwani pamoja na Rais
wetu Dk. John Pombe Magfuli kwa kuwaleta wawekezaji hawa ambao watatusaidia
kuondokana na tatizo la kupata soko la uhakika,”walisema wakulima hao.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka maafisa kilimo wote kuhakikisha
wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwasimamia vema wakulima wa zao hilo la
muhogo kutonyonywa na walanguzi na kupata haki zao stahiki na
kuahidi kuwaondoa kazini wale wote ambao watabainika kukwamisha juhudi za
serikali katika uwekezaji wa sekta ya viwanda.
Aidha Ndikilo alisema kuwa lengo kubwa
la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawasaidia kwa hali na mali
wananchi wake katika kuondokana na changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili
ikiwemo ukosefu wa masoko ya uhakika na ajaira, hivyo atahakikisha zao hilo la
muhogo linapata soko kupitia viwanda ambavyo vinajengwa na wawekezaji katika
maeneo mbali mbali na kuwahimiza wasikate tamaa na badala yake waendelee zaidi
kulima mazao ya biashara ikiwemo ufuta, muhogo na korosho.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Mkuranga Filberto Sanga amesema kuwa kipindi cha nyuma wakulima
wengine walikuwa tayari wameshakata tamaa katika kilimo cha
zao la muhogo, hivyo kukamilika kwa kiwanda hicho kitaweza kuleta mabadiliko
chanya kwa kuwapa fursa wananchi kuwa na soko la uhakika.
“Kwa kweli wananchi wangu hasa kwa
wakulima wa zao hili la muhogo katika Wilaya ya Mkuranga baadhi yao walikuwa
tayari wameanza kukata tamaa kabisa kutokana na mfumo ambao ulikuwepo wanauza
mazao yao kwa bei ya hasara lakini kwa sasa kiwanda hiki kinachotarajiwa
kukamilika mwaka huu wataondokana kabisa na changamoto ya soko,” alismema
Sanga.
Awali akisoma Risala ya ujenzi wa mradi
huo mmoja wa vongozi wa kiwanda hicho, Leonard Jambeli
kwa niaba ya Mkurugenzi amebainisha kwamba waanategemea kutoa fursa za
ajira za moja kwa moja kwa wazawa zaidi ya mia moja pindi uzalishaji
utakapoanza kufanyika rasmi.
Kukamilika kwa mradi huo wa ujenzi wa
kiwanda mwishoni mwa mwaka huu kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa
wakulima wa zao hilo katika halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani
ambao kwa miaka mingi walikuwa wanapata hasara kutokana na kunyonywa na
walanguzi kununua zao hilo kwa bei ndogo.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa
wa Pwani kushoto Ramadhani Maneno akimshika mkono Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarist Ndikilo ikiwa ni moja ya ishara ya kumpongeza katika juhudi
zake za kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani kushoto Mhandisi
Evarist Ndikilo akipata maelekezo kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha
kuchakata muhogo wakati alipofanya ziaara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweka
jiwe la msingi katika kiwanda hicho, (PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)