Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum
akionyesha gazeti la Tanzania Daima kwa waandishi wa habari.
....................................
Viongozi
wa Dini nchini, wamesema Rais JOHN MAGUFULI Hajakataa kuzungumza wala kuwapuuza
viongozi hao ambao wamemuomba kukutana naye, kama inavyoenezwa na baadhi ya
vyombo vya habari.
vyombo vya habari.
Akizungumza
leo jijini, Dar es Salaam na waandishi wa habari Sheikh wa Mkoa wa Dar es
Salaam Alhad Mussa Salum, amesema taarifa zilizochapishwa na gazeti la Tanzania
Daima la Septemba 21 ISSN 0856 9762 toleo na.4310 sio za kweli.
“taarifa
hizo sio za kweli, taarifa hizo zimelenga kumgombanisha Rais na Viongozi wa
Dini na watanzania kwa ujumla na hilo halitafanikiwa,” alisema Sheikh Alhad.
Aidha
Viongozi hao wamesema uamuzi wao wa kumuomba Rais kuonana naye, haujatokana na
kuagizwa na UKAWA, bali umetokana na maono waliyopewa na Mwenyezi Mungu.
Amefafanua
kuwa Rais MAGUFULI anawaheshimu Viongozi wa dini na mara zote amekua akiwaomba
wamuombee na kusema leo ni siku ya tano tangu wamuandikie barua ya kumuomba
kukutana naye na wanaimani Rais atakutana na Viongozi hao.
Ameeleza
kuwa Barua hiyo imeandikwa Septemba 19 na kupelekwa siku hiyo hiyo Ikulu, ikiwa
imesainiwa na Katibu Mkuu wa Bakwata, Katibu Mkuu wa CCT na Katibu Mkuu wa TEC.
“Naomba
watanzania wasisikilize maneno hayo kwasababu hayana nia njema kwa Taifa letu,
naamini Mh Rais tutaonana nae na tutaongelea mustakbali wa nchi katika mambo
mbalimbali,” alisistisa Sheikh Alhad
Akizungumzia
utendaji wa Serikali ya Rais MAGUFULI, Sheikh ALHAD amesema Rais amerejesha
nidhamu Serikalini, ukusanyaji mapato umeimarika na pia pengo kati ya
wasionacho na walionacho linaanza kupungua.
No comments:
Post a Comment