Mkuu wa
Polisi wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP, Adam Maro, mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, wakufunzi wa Mgambo Bagamoyo, pamoja
na Mgambo kutoka kata mbalimbali za Bagamoyo, wakifurahipamoja kwa kuimba nyimbo za gwaride mara baada ya kufanya
usafi siku ya tarehe 1 Septemba.
Sajenti Mwasimba, kutoka jeshi la nchi kavu makao
makuu, akiwa amechuchumaa kwa mzuka wakati akiwaimbisha nyimbo mgambo wilayani
Bagamoyo, katika maadhimisho ya miaka 52 ya
JWTZ.
Mgambo wilayani Bagamoyo, wakiwa imara kupokea
maelekezo kutoka kwa wakufunzi wao,
wakiwa wamebeba mafagio Reki, na Kwanja, kwaajili ya usafi siku ya maadhimisho
ya miaka 52 ya JWTZ, Septemba mosi.
Mgambo wilayani Bagamoyo, wakiwa imara kupokea
maelekezo kutoka kwa wakufunzi wao,
wakiwa wamebeba mafagio Reki, na Kwanja, kwaajili ya usafi siku ya maadhimisho
ya miaka 52 ya JWTZ.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga akihojiwa na waandishi wa Habari huku akiwa juu ya Trekta la kubebea taka siku ya maadhimsho ya miaka 52 ya JWTZ Septemba mosi.
.....................................
Mwenyekiti wa kamati ulinzi na usalama wilaya ya Bagamoyo,
majid Mwanga, amesema matukioya uhalifu wilayani humo yamepungua ukilinganisa na kipindi cha nyuma.
Majid Mwanga ambae pia nia ni mkuu wawilaya ya
Bagamoyo, alisema hali ya kupungua kwa uhalifu katika wilaya ya Bagamoyo,
imetokana naushirikianouliopo katiyawananchi na vyombo vya ulinzina usalama
ambapo raia wema wamekuwa wakitoa taarifa za kuwepo kwa wahalifu na kufanikisha
kukamatwa.
Hayo aliyasema wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya
Jeshi la Wananchi wa Tanzania siku iliyoadhimishwa kwa kwa kufanya usafi ambapo
kwa Bagamoyo Jeshi la akiba (Mgambo) lilitumika kutekeleza usafi huo huku mkuu
wa wilaya akishiriki kwa kuendesha Trekta la kubebea taka kuanzia asubui mpaka
jioni.
Aidha, aliwataka wananchi wilayani humo kuwa wazalando kwa kuipenda
nchi yao na kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani ambavyo vitakavyopelekea serikali
kutumia nguvu kukabiliana navyo na kusababisha hasara kwa taifa mahusiano mabaya kati ya wananchi
na serikali yao.
Alisema, wanaofanya vitendo vya uvunjifu wa
amanai siku zote ni
watu wachache, serikali inapotumia
nguvu kupambana nao wataathirika
na wananchi wasiokuwa na hatia jambo ambalo linaweza kuleta uhasama
miongoni mwa vikosi vya ulinzi na usalama.
Diwani, wa kata ya Kiromo Mh. Hassani R. Usinga. (Wembe).
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kiromo, Hassani
Usinga (Wembe) aliwataka mgambo kuwa wazalendo ili serikali ifaidike nakuwepo
kwajeshi hilo la akiba, kwa kushiriki katika
matukiombalimbali pale wanapohitajika.
Alisema sivyema kumuona mgamboanaitwa akatekeleze
majukumu yake halafu anakwepa jambo
ambalo halitakiwi kwa mgambo aliyekula kiapo cha utii na uwajibikaji katika shughuli za
kitaifa.
Aliongeza kuwa, mgambo ni jeshi la akiba ambaloserikali za kata
zinawategemea kuimarisha ulinzi katika kata zao hivyo wakinesha nidhamu na
uwajibikaji serikali za kata zinaweza kuwajengea vituovitakavyotoa huduma ya ulinzai
kwa jamii.
Alisema tayari yeye katika kata ya Kiromo
ameandaa mpango wa kujenga kituo ambapo mgambo watakaa hapo ili kurahisisha
shughuli za ulinzi na usalama.
Akizungumzia hali ya usafi katika mji wa Bagamoyo mkuu huyo wa wilaya
aliwataka wananchi kudumsha usafi ili kuepuka magonjwa mbalimbali ya kuambukiza,
na kusisitiza kuwa usafi wa pamoja katika mji wa Bagamoyo
utafanyika mara mbili kwa mwezi.
Kufuatia mkakati huo wa kufanya usafi wa pamoja
mara mbili kwa mwezi, mkuu huyo wa wilaya aliwaagiza mgambo kuwakamata watu
wote watakaofungua biashara zao katika siku zilizotangazwa kufanya usafi.
Aidha, alimuagiza Afisa mazingira wilaya ya
Bagamoyo,kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote ambao hawajaweka vifaa vya
kutupia taka kwenye maeneo yao ya kufanyia biashara vinginevyo atamuwajibisha
yeye.
Mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga akiwa na katibu tawala wa wilaya, Erica
Lyegela wakipita mitaani kukusanya taka
na Trekata na kwenda kuzimwaga Dampo, katiKa maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ. Septemba mosi.

wilaya ya Bagamoyo, ambae piya ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya, Majid Mwanga
mwenye miwani kushoto akipiga kwata pamoja na
mgambo na kwanja lake begani,
ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, Septemba
mosi.

Mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na Usalama wilaya, Mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga,
kulia, pamoja nae mkuu wa polisi wilaya ya Bagamoyo, mrakibu Mwandamizi wa Polisi,
SSP-Adam Maro wakiimba na kucheza pamoja na mgambo siku ya maadhimisho ya miaka
52 ya JWTZ, Septemba mosi.
Ni siku ya sherehe baada ya usafi viongozi
walishiriki na mgambo kuimba nyimbo na kucheza pamoja, Klia ni Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na Usalama wilaya,
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid mwanga, wa tatu kulia mwenye sare za polisi ni mkuu wa Polisi
wilaya ya bagamoyo, mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP- Adam Maro kwa mbali
anaonekana Afisa tarafa wa Yombo Mzee Kidelenya, Kushoto ni katibutawala wa
wilaya ya Bagamoyo, Bi, Erica Lyegela wakiongozwa kwa nyimbo na Mkufunzi wa Mgambo kutoka Jeshi la nchi kavu makao makuu ya jeshi, Sajenti
Mwasimba, ambae yupo mbele yao.
Mgambo wilayani Bagamoyo, wakiwa imara kupokea
maelekezo kutoka kwa wakufunzi wao,
wakiwa wamebeba mafagio Reki, na Kwanja, kwaajili ya usafi siku ya maadhimisho
ya miaka 52 ya JWTZ, Septemba mosi.
Mgambo wilayani Bagamoyo, wakiwa imara kupokea
maelekezo kutoka kwa wakufunzi wao,
wakiwa wamebeba mafagio Reki, na Kwanja, kwaajili ya usafi siku ya maadhimisho
ya miaka 52 ya JWTZ, Septemba mosi.
Mgambo wilayani Bagamoyo, wakiwa imara kupokea
maelekezo kutoka kwa wakufunzi wao,
wakiwa wamebeba mafagio Reki, na Kwanja, kwaajili ya usafi siku ya maadhimisho
ya miaka 52 ya JWTZ, Septemba mosi.
Mgambo wilayani Bagamoyo, wakiwa imara kupokea
maelekezo kutoka kwa wakufunzi wao,
wakiwa wamebeba mafagio Reki, na Kwanja, kwaajili ya usafi siku ya maadhimisho
ya miaka 52 ya JWTZ, Septemba mosi.
Mgambo wakiendelea na usafi katika mitaa ya Bagamoyo
wakati wa maadhimisho wa ya miaka 52 ya JWTZ.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo majid Mwanga akibinua
tera la taka, eneo la kutupia taka.
Mgambo wakirejea ofisi ya mkuu wa wilaya mara
baada ya kumaliza kufanya usafi.
Mgambo wakiwa wamewasili ofisi ya mkuu wa wilaya
wakiongozwa na Mkufunzi wao kutoka jeshi
la nchi kavu kutoka makao makuu ya
jeshi Sajenti Mwasimba.
Mkuu wa Polisi wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu mwandamizi wa
Polisi, SSP- Adam Maro, akiwa anasisitiza jambo wakati akizungumza na mgambo
katika Ofisi ya mkuu wa wilaya.
Katibu tawala wilaya ya Bagamoyo, Erica Lyegela,
akiangalia mazingira ya usafi katika
ofisi ya mkuu wa wilaya.
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo,
Majid Mwanga akisisitiza kwamba
usafi pamoja Bagamoyo ni siku 2
kwa mwezi.
No comments:
Post a Comment