Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara Gonzalez
akielezea jinsi wanafunzi hao 10 watakavyoweza kufaidika na udhamini wa Mo
Dewji Foundation.
.........................................................
Mo Dewji Foundation kwa kushirikiana na
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – UDSM Imezindua rasmi mpango wa ufadhili kwa
wanafunzi 10 wa elimu ya juu waliomaliza kidato cha sita mwaka huu wa 2016 (MO
Scholar Program) kwa chuo kikuu cha Dar es salaam leo Jumatano Septemba, 7
2016.
Mpango huu wa ufadhili kwa wanafunzi
umelenga kuwawezesha wanafunzi wenye sifa tatu, wasio na uwezo wa kujilipia ada
ya chuo, wanafunzi ambao wameshiriki vyema katika michezo na uongozi wakiwa
shuleni na wanafunzi ambao wamefaulu kwa kiwango cha alama 1 na 2 (division 1
& 2)
Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara
Gonzalez amesema kuwa wameanzisha mpango huo kwa lengo la kusaidia sekta ya
elimu nchini Tanzania kwa kutoa msaada wao wa udhamini wa elimu ya juu kwa
wanafunzi waliomaliza kidato cha sita.
“Mpango wetu kwa muda wa miaka mitatu hadi
minne ni kusaidia zaidi Tanzania lakini hapo baadae kama tukifanikisha malengo
yetu Tanzania tutakwenda mbali zaidi,” ameongeza Barbara.
Aidha Mkurugenzi wa masomo ya shahada za
awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Allen Mushi ameelezea kuwa
chuo kikuu cha Dar es salaam kimelenga kusaidia wanafunzi wote wa kitanzania
ambao wanasifa za uhitaji wa ufadhili na ameomba vyombo vya habari visaidie
kusambaza ujumbe kwa watanzania ili wanafunzi wafaidike na mpango huo.
“Tumeanza na chuo Kikuu cha Dar es salaam,
tutaangalia namna ambavyo mpango na tutaenda na hapo baadae tutatanua mikono
yetu kwenda vyuo mbalimbali,” amesema Barbara.
Na kwa mtahiniwa ambaye anakuwa anahitaji
kutuma maombi kwa ajili ya kupata ufadhili wa Mo Dewji Foundation kwa ajili
masomo ya chuo kikuu anaweza kuingia tovuti ya modewjifoundation.org
Mkurugenzi wa masomo ya shahada za awali katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Allen Mushi akizungumzia mchakato wa
kupata wanafunzi 10 ambao watapata udhamini wa Mo Dewji Foundation.
No comments:
Post a Comment