Wafugaji na wakulima wakiwa kwenye mkutano wa
pamoja ulioitishwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid hemed mwanga.
Meza kuu, Kutoka kushoto mkurugenzi Halmashauri
ya Chalinze, Edes Lukoa, wa pili kushoto
ni mwenyekiti wa kikao hicho mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, wa tatu kutoka kushoto ni Mbunge wa
jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Jumanne
Kawambwa, na wa kwanza kulia ni kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Bagamoyo, Dkt. Amiri Batenga.
..........................
Mkutano huo umeitishwa ili kujadili migogoro
baina yao, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha uongozi wa elimu Bagamoyo (ADEM) umewajumuisha
wenyeviti wa vijiji wote, watendaji kata wote, maafisa tarafa wote, maafisa
kilimo na mifugo wa kata zote zawilaya ya Bagamoyo pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya
wilaya.
Lengo la kikao hicho ni kutafuta ufumbuzi wa migogoro inayotokea mara kwa mara kati ya
wakulima na wafugaji ambapo hivi kari
buni kumeripotiwa matukio ya mapigan na
kutishiana amani b aina ya pande
hizo mbili.
Migogoro hiyo pamoja na madhara mbalimbali
yaliyotokea ikiwemo wakulima kukimbia mashamba yao, wafugaji nao
kupoteza mifugo yao pia imepelekea kuuwawa kwa mfugaji katika kata ya
Makurunge, na mama mmoja mkulima kuuwawa kwa
kukatwa katwa na mapanga na
hatimae kumtia ndani ya shimo la
choo huko kata ya miono.
Kufuatia hali hiyo ilimulazimu mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bagamoyo ambae
ndiye mkuu wa wilaya kuitisha kikao cha
pamoja ili kutafuta ufumbuzi.
Katika kikao hicho kilichodumu kwa muda wa saa 10 kuanzia saa 4 asubuhi
mpaka saa 1 usiku, kilitoka na maazimo
18 ambayo yanahitajika kutekelezwa ili kuepuka migogoro hiyo isijirudie.
Wakulima na wafugaji wakifuatilia yanayoendelea
katika kikao hicho
Wakulima na wafugaji wakifuatilia yanayoendelea
katika kikao hicho
Wakulima na wafugaji wakifuatilia yanayoendele
katika kikao hicho
Wakulima na wafugaji wakifuatilia yanayoendele
katika kikao hicho
Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bagamoyo
ikifuatilia yanayoendelea katikakikao hicho
Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bagamoyo
ikifuatilia yanayoendelea katikakikao hicho
Mtaalamu kutoka idara ya Ardhi Mosesi Kibona
akitoa elimu juu matumizi bora ya Ardhi katika kikao hicho
Wataalamu
kutoka Halmashauri ya Bagamoyo wakifuatilia kwa makini yanayoendelea
katika kikao hicho, wa kwanza kulia
ni Mchumi- idara ya Mipango Halmashauri
ya Bagamoyo, Jalala Samata na watatu kutoka kulia ni Afisa Mifugo kutoka idara
ya Mifugo Bagamoyo, Sinani R. Simba.
Mwenyekiti wa chama cha wafugaji mkoa wa Pwani,
Mohamedi Geboe akielezea changamoto
wanazokumbana nazo wafugaji.
Afisa Mifugo kutoka idara
ya Mifugo Bagamoyo, Sinani R. Simba, akifafanua sheria ya mipango miji kuhusu mifugo
Katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo, Erica Lyegela
akitoa muongozo wa kikao hicho
Mwenyekiti wa mkutano huo, mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo, Majid Hemedi Mwanga akisikiliza kwa makini hoja na maoni ya pande
zote katika kikao hicho ambacho
kimelenga kumaliza migogoro ya
wakulima na wafugaji wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa Polisi wilaya ya kipolisi Chalinze, Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi, SSP- Janeth Magomi, akielezea idadi ya kesi, kati ya wakulima na
wafugaji zilizoripotiwa polisi katika Halmashauri ya Chalinze.
Mkuu wa Polisi wilaya ya kipolisi Bagamoyo, Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi, SSP- Adam A. Maro, akielezea idadi ya kesi kati ya wakulima na
wafugaji zilizoripotiwa polisi katika Halmashauri ya Bagamoyo.
Wakulima na wafugaji wakifuatilia yanayoendele
katika kikao hicho
Maafisa tarafa wakifuatilia kwa makini
yanayoendelea katika kikao hicho.
Maafisa tarafa wakifuatilia kwa makini
yanayoendelea katika kikao hicho.
No comments:
Post a Comment