Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella
Kairuki akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu
zoezi la utambuzi na usajili wa vitambulisho kwa watumishi wa umma litakaloanza
tarehe 03 Oktoba. Kulia kwaker ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurian
Ndumbaro na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Seerikali Mtandao (EGA), Dkt.
Jabir Bakari
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulkisho vya Taifa (NIDA), Mohammed Khamis
Abdallah akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam, kuhusu zoezi la utambuzi na usajili wa vitambulisho kwa watumishi wa
umma litakaloanza tarehe 03 Oktoba . Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Seerikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir
.....................................
SERIKALI inatarajia kufanya zoezi la utambuzi na usajili wa taarifa za
watumishi wa umma kuanzia tarehe 3 Oktoba ili kutoa vitambulisho vya Taifa
vilivyo na taarifa zote muhimu za mtumishi husika.
Hayo yamebainisha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki alipokutana na waandishi wa
habari ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Kairuki amesema kuwa zoezi hilo la utambuzi na usajili wa wananchi ambalo
linaanza na watumishi wa umma ni muhimu na litasaidia kupunguza gharama kwa
Serikali na kuondoa usumbufu kwa wananchi kwani taarifa zao zote muhimu
zitakuwa sehemu moja hivyo kupunguza kero ya kuulizwa taarifa kila uendapo.
Waziri Kairuki amesema kuwa zoezi hilo litashirikisha Wizara yake pamoja
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA), ambapo taarifa zitakazotumika ni zilizilizopo katika vitambulisho
vya mpiga kura.
“Kama mnavyofahamu kuwa Serikali ipo katika maboresho makubwa ya utendaji
wake, hivyo ili kuendana na hali hiyo tutaanza zoezi la utambuzi na usajili wa
watumishi wa umma kuanzia tarehe 3 Oktoba, zoezi litakalochukua takribani wiki
mbili, zoezi hili ni muendelezo wa Serikali kukabiliana na matatizo ya kutokuwa
na taarifa sahihi.” Alisema Kairuki.
Aidha Kairuki amewata watumishi wote wa umma kushiriki zaoezi hilo wakiwa
na taarifa zote muhimu zinazowatambulisha ambazo ni pamoja na Cheti cha
kuzaliwa, vyeti vya elimu, kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Mzanzibar Mkazi,
hati ya malipo ya Mshahara, hati ya kusafiria na kadi ya mpiga kura.
Waziri huyo ametoa wito kwa waajiri kuweka mazingira wezesha ili
kufanikisha zoezi hilo ikiwemo kutenga ofisi itakayotumiwa na kwa kazi hiyo
pamoja na kusisitiza waajiri wahakikishe watumishi wao wanasajiliwa bila kukusa
na taarifa ya zoezi hilo iwasilishe Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawabora ndani ya siku 14 tangu zoezi hilo kukamilika kwake.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Dkt. Laurian Ndumbaro amewataka watumishi wote wa umma
kulipa umuhimu mkubwa zaozi hilo na kusisitiza kuwa Serikali haita sita
kucghukua hatuia za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma kwa
mtumishi yeyote atakaye kaidi zoezi hilo.
Awali akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu namna zoezi hilo
litakavyotekelezwa nchi znima kwa muda wa wiki mbili tu, Kaimu Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mohammed Khamis Abdallah amesema kuwa
zoezi hilo litafanikiwa kwani wanao wafanyakazi zaidi ya 460 nchini nzima ambao
wapo katika Ofisi za Halmashauri.
Pia aligusia suala la vifaa na kusema kuwa tayari wamewasiliana na Tume
ya Taifa ya Uchaguzi ambayo imewapa mashine za BVR kwa ajili ya kuzitumia
katika zoezi hilo la utambuzi na usajili.
Zoezi la utambuzi na usajili wa wananchi hasa watumishi wa uuma
kukabiliana na vyanzo vya watumishi hewa kwa kuunganisha mifumo ya utambuzi wa
watu na mifumo mingine ikiwemo usimamizi wa rasilimali watu na mishahara katika
utumishi wa umma ambapo kuunganishwa kwa mifumo hiyo kutawezesha mifumo hiyo
kuwasiliana na kutumia taarifa zilizo kwenye kanzi data ya NIDA suala
litakalokuwa limerahisisha upatikanaji wa taarifa.
No comments:
Post a Comment