Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akikata utepe kuzindua
mpango huo kwa ajili ya mikoa ya Iringa na Njombe katika viwanja vya
Mwembetogwa mjini Iringa
....................................
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amesema
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwasajili watoto wote nchini wenye umri
chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa.
Dhamira hiyo ya Serikali inalengo la kuiondoa nchi katika takwimu
zinazoonyesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwisho barani Afrika ambazo
watoto hawana vyeti vya kuzaliwa.
Dkt Mwakyembe amesema hayo mjini iringa alipokuwa akizindua kampeni ya
uandikishaji watoto chini ya miaka mitano katika mikoa ya Iringa na Mbeya
iliyofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa.
Dkt Mwakyembe ameelezea kusikitishwa na kitendo hicho cha kuwa miongoni
mwa nchi ambazo watoto wake hawajasajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa na
kusema kuwa ndio maana kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikaamua kuendesha
kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano.
Amesema serikali imedhamiria kuiondoa Tanzania katika hali hiyo kwakuwa
sio sahihi kwa nchi kuwa katika nafasi hiyo sawa na Somalia
‘Hali hii sio sahihi, Tanzania haistahili kuwepo katika kundi hilo
tumedhamiria kuiondoa nchi huko, tunataka Tanzania iwe juu ktk usajili wa
watoto kama ilivyo juu kwa chanjo mbalimbali kwa watoto wetu’ alisema.
Mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuhakikisha watoto wote
chini ya miaka mitano wanasajiliwa na kuwa ma vyeti vya kuzaliwa unaendeshwa
kupitia Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi RITA chini ya ufadhili wa
UNICEF.
No comments:
Post a Comment