Maofisa
na Askari wa Jeshi la Magereza wakipunga mikono ikiwa ni ishara ya kuwaaga
Wastaafu hao wakati wakipita katika magari Maalum (hawapo pichani).
Wastaafu
wa Jeshi la Magereza wakiwasili katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya
Urekebishaji, Ukonga, Dar es Salaam wakiwa wameongozwa na Kamishna Mstaafu wa
Magereza Deonice Chamulesile wakielekea Jukwaa Kuu kupokea Salaam ya Heshima.
Hafla ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi la Magereza imefanyika leo Septemba 23,
2016.
Kamishna
Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akiwa katika Jukwaa Kuu akipokea Salaam
ya Heshima kutoka kwenye Gwaride Maalum la kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la
Magereza.
Kamishna
Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akikagua Gwaride Maalum la kuwaaga
Wastafu wa Jeshi la Magereza lililoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza.
Gwaride
Maalum likipita mbele ya Jukwaa kwa Heshima.
Viongozi
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakipiga Saluti wakati Gwaride Maalum likipita
mbele ya Jukwaa kwa heshima. Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Kamishna
Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akiwa pamoja na Wastaafu wengine wa
Jeshi la Magereza wakitoa Salaam za mwisho wakiwa kwenye magari wakati Gwaride
Maalum likiwa limeunda Umbo la OMEGA.
Kamishna
Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile(katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Wastaafu wa Jeshi la Magereza pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi
la Magereza(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza,
Dkt. Juma Malewa(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment