Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari LEO
jijini Dar es Salaam kuhusu kampeni ya kupima afya bure ambayo inaratibiwa na
ofisi yake kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Hospitali za
rufaa za Mkoa wa Dar es Salaam na Afya Check ya Clouds FM pamoja na wadau
wengine. Kampeni ya kupima afya itafanyika Septemba 24 na 25, mwaka huu kwenye
viwanja vya Mnazi mmoja siku ya Jumamosi na Jumapili.
..................................
TAARIFA YA MKUU WA MKOA MH. PAUL MAKONDA
Napenda nichukue fursa hii kuwajulisha kuwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam imeandaa zoezi la kiafya kwa wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam
linalotarajia kufanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 24/09/2016 siku
ya Jumamosi na tarehe 25/09/2016 siku ya Jumapili kuanzia saa mbili kamili
asubuhi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Ndugu Wananchi,
Napenda kuwajulisha kuwa hii ni habari njema kwetu kwani huduma zote za
vipimo zitatolewa bure bila gharama yoyote hivyo tunaombwa kushiriki kikamilifu
katika zoezi hili la kuzijua vema afya zetu kwani itatuwezesha kijikinga na
magonjwa yanayoweza kijitokeza, kuepuka matumizi ya gharama kubwa za matibabu,
na kuzuia vifo visivyo vya lazima kwani kuna wengine huenda hospitali pindi
hali imekua mbaya sana.
Ndugu Wananchi,
Napenda kuwajulisha kuwa KILA AINA YA UGONJWA KATIKA MAGONJWA KUMI
MAKUBWA kama vile Shinikizo la Damu, Kisukari, Saratani ya Matiti, Saratani ya
Shingo ya Uzazi, Tezi Dume, Saratani ya ngozi kwa albino na Magonjwa mengine
mengi yatapimwa.
Hivyo wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam mnahamasishwa kufika kwa wingi
kwani MADAKTARI BINGWA kutoka HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, TAASISI YA SARATANI
YA OCEAN ROAD, TAASISI YA MOYO YA JAKAYA MRISHO KIKWETE, HOSPITALI ZA RUFAA ZA
MKOA WA DAR ES SALAAM, HOSPITALI YA AGAKHAN, TAASISI ZA CCP MEDICENE wote kwa
pamoja watakuwa tayari kuwahudumia.
Ndugu Wananchi,
Ninaimani ya kuwa kila mmoja wetu anajua umuhimbu wa AFYA YAKE kwani
utakapoijua vema afya yako itakusaidia kuwa salama kila iitwapo leo na
kukupelekea kuwa na nguvu ya kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato cha
kila siku sambamba na kuinua uchumi wa Taifa letu la Tanzania.
CHEKI AFYA YAKO KWA UBORA WA MAISHA YAKO
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA
Paul C. Makonda
MKUU WA MKOA WA
DAR ES SALAAM
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Onesmo Kisanga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) LEO akizungumzia kuhusu umuhimu wa kupima afya mara kwa mara ili kuzuia
uwezekano wa mtu kupata matatizo makubwa ya magonjwa ya figo.
Baadhi
ya waandishi wa habari na madaktari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda wakati akiwahamasisha wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na
mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kupima afya Septemba 24 na 25, mwaka huu.
Kutoka
kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ilala, Victoria Ludovick, Daktari Bingwa
wa Magonjwa ya Figo, Onesmo Kisanga wa Muhimbili na Mshauri Mtaalamu wa
Uchunguzi wa Magonjwa ya Figo, Dk Omar Sherman wa Hospitali ya Aga Khan
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda LEO.
Mkurugenzi
wa Huduma za Tiba Shirikishi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk
Praxeda Ogweo amewataka wananchi kujenga tabia ya kupima afya hasa kina mama
kupima endapo wanaviashiria vya kansa au la.
Mganga
Mkuu wa Kinondoni, Dk Aziz Msuya akizungumza katika mkutano wa kuwahamasisha
wananchi kujitokeza kwa wingi katika kampeni ya kupima afya ambayo itafanyika
Septemba 24 na 25, mwaka huu.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na wataalamu wa afya wa jijini Dar es Salaam Leo. Kutoka kulia ni
Mshauri Mtaalamu wa Uchunguzi wa Magonjwa ya Figo, Dk Omar Sherman wa Hospitali
ya Aga Khan, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Onesmo Kisanga wa Muhimbili,
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili, Dk Hedwiga Swai, Mkuu wa Idara ya
Magonjwa ya Dharura na Ajali Muhimbili, Dk Juma Mfinanga na Mganga Mkuu wa
Kinondoni, Dk Aziz Msuya.
No comments:
Post a Comment