Mmoja
wa wakurugenzi wateule Bw.Hudson Stanley Kamoga Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu,
ambae kitaaluma ni mtangazaji.
.................................
Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Manispaa na Wilaya,
walioteuliwa siku ya Jumamosi Septemba 10, 2016 na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wametakiwa
kuwasilisha nakala halisi za vyeti vyao vya taaluma, kabla ya kuapa.
Zoezi la uhakiki wa vyeti hivyo litakalofanyika Ofis ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika jengo la Mkapa mjini Dodoma siku
ya Jumanne Septemba 13, 2016 kabla ya kuanza kwa zoezi la kuapa.
Wakurugenzi hao 13 ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa mmoja, Mkurugenzi wa Mji mmoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za
Wilaya 11, wanatakiwa kuwasili Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma saa 2:00
asubuhi kwa ajili ya uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI
Mhandisi Mussa Iyombe na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Rebecca Kwandu, Septemba 11, 2016 inawataka
Wakurugenzi hao kuhakikisha wanawasilisha nakala halisi ya vyeti vyao vya
taaluma kwa ajili ya kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma,
unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki
kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi yaani vivuli.
Wakurugenzi hao ni Godwin Emmanuel Kunambi Manispaa ya Dodoma, Elias R.
Ntiruhungwa Mji waTarime, Mwantumu Dau Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Frank
Bahati Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Hudson Stanley Kamoga
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mwailwa Smith Pangani, Halmashauri ya Wilaya ya
Nsimbo, Godfrey Sanga, Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama na Yusuf Daudi
Semuguruka Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.
Wakurugenzi wengine ni Bakari Kasinyo Mohamed Halmashauri ya Wilaya ya
Nachingwea, Juma Ally Mnweke Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Butamo Nuru
Ndalahwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Waziri Mourice Halmashauri ya Wilaya
ya Karatu na Fatma Omar Latu Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment