Katibu
Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Erica Yegella akizungumza na wajumbe
wa mabaraza ya ardhi na nyumba ngazi ya kata hawapo pichani katika
ufunguzi wa kikao kazi maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa
kutekeleza majukumu yao katika kutatua migogoro ya ardhi kilichofanyika katika
shule ya sekondari Lugoba.
NA VICTOR MASANGU.
WATUMISHI wa umma Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wametkakiwa
kuachana na vitendo vya kuwa na tamaa, ya kupokea rusha au kutoa kwa lengo la
kuweza kuuza viwanja kiholela bila ya kuzingatia sheria na utaratibu kwani
kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha kuwepo migogoro
ya ardhi ya mara kwa mara kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Erica Yegella kikao
maalumu cha mafunzo ya kazi kilichoandaliwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo
wa kuweza kutimiza majukumu yao ipasavyo wajumbe wa mabaraza ya ardhi na
nyumba ngazi ya kata zilizopo katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Yegella alisema kwamba watendaji wa ngazi zote kwa kushirikiana na
wajumbe wa mabaraza wanapaswa kuitambua vizuri sheria ya ardhi ambayo itaweza
kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua migogoro ambayo imedumu kwa
kipindi cha muda mrefu ikiwa sambamaba na kutenda haki bila ya kuwa na
upendeleo wowote ili kuepukana na vurugu ambazo zinapelekea uvunjifu wa amani.
“Jamani nyinyi ni watendaji hivyo ni lazima kuhakikisha mnafanya kazi kwa
misingi ambayo inatakiwa kitendo cha kuuza mashamba au vinnja ni kinyume kabisa
na sheria, na kingine tuache tama kabisa ya kufanya mambo bila kuangalia
madhara yake kwani baadhi ya maeneo migogoro ya ardhi inachangiwa na baaadhi
yetu,”alisema Yegella.
Aidha alisema kwamba ana imani baada ya watendaji hao kupatiwa mafunzo
hayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kutatua migogoro ya ardhi
ambayo wakati mwingine inapelekea kuwepo kwa vurugu kutokana na kugombania
viwanja.
Naye Afisa kutoka tume ya maadili ya viongozi wa umma kanda
ya Mashariki Seleman Shaban amewataka watendaji nawatumishi wa umma kuhakikisha
wanazingatia maadili na taraibu zote za kazi zao ili kuepukana na suala
la kutoa au kupokea rushwa kwani ni kinyume kabisa na sheria za nchi.
Jerome Njiwa ni Mwenyekiti wa baraza la ardhi katika Wilaya ya Kibaha
ambaye alihudhuria katika kikao hicho na hapa anafafanua zaidi kuhusina na
migogoro mingi ambayo imekuwa ikijitokeza katika mabaraza ya ardhi ya kata na
nyumba kutokana na kutozifahamu sheria vizuri.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata
na nyumba warioshiriki katika mafunzo hayo akiwemo Mwinyikondo Asia,
Mariamu Swala pamoja na Hassan Ally wamesema kwamba walikuwa wanakabiliwa na
changamoto nyingi katika ufanya maamuzi kutokana na kutozijua vizuri sheria za
ardhi.
Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wamewashirikisha wajumbe mbali
mbali kutoka katika mabaraza ya ardhi ya kata zilizopo katika
Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweza kupunguza kero na
migogoro ya aradhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara na kusababisha
vurugu kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment