Mkuu wa wilaya ya handeni Mh.Gondwe akizungumza na wananchi wa vijiji
vya nyasa na madebe akiwakataza wasiuze ardhi kiholela na wasigombanie maeneo kwaajili ya kutaka kuyauza.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Gondwe akipeana mkono wa pongezi na
Mwenyekiti wa kijiji cha Nyasa baada ya kutatua mgogorowa mpaka wa maeneo yao.
Mkuu wa wilaya Mh.Godwin Gondwe akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya Handeni,Ndugu William Makufwe (pichani kushoto) akitoa ufafanuzi
kwa wananchi wa vijiji vya nyasa na madebe.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe
akisalimiana na mkazi wa kijiji cha nyasa.
Mkuu waa Wilaya ya Handeni,Mh Godwin
Gondwe Jana alifanikiwa kusuluhisha mgogoro wa mpaka uliokuwa
ukivihusisha vijiji viwili vya kata ya kang’ata wilayani Handeni.
Vijiji hivyo ni
Madebe na Nyasa ambao walikua hawafahamu mpaka wao unaishia wapi,suluhu hiyo
ilifanikiwa kumalizwa na mkuu wa wilaya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri
ya wilaya ya Handeni ,Bwa.William Makufwe.
DC Gondwe pia aliwataka wananchi na viongozi
wajikite katika shughuli za kimaendeleo badala ya kujikita kwenye suala la
mipaka ,Kwa madai wapate maeneo ya kulima wakati wakigombania maeneo ili
wauze.
Aidha, amewaonya wasiuze ardhi kiholela na kufanya vizazi vijavyo kuwa
watumwa kwenye ardhi yao.
No comments:
Post a Comment