Mwenyekiti
wa The Islamic Foundatio, Aref Nahdi, kulia akiwa na Muft Ismail Menk wa Zimbabwe
Mwenyekiti
wa The Islamic Foundation
Aref Nahd
Mufti,
Ismaili Menki wa Zimbabwe
............................................................
Waislamu wametakiwa kuishi katika dunia kama wapo shuleni ili
kutekeleza malengo maalum ya kuumbwa kwa binadamu hapa duniani.
Wito huo umetolewa jijini Dar
es Salaam, na Mufti wa Zimbabwe Sheikh, Dkt. Ismail Menk, alipokuwa akitoa hutuba
katika ukumbi wa Diamond Jublee ambapo amewataka waislamu
kutambua kwamba yapo maisha mengine baada ya
kufa.
Alisema mtu anapokufa ataulizwa kuhusu maisha yake ya duniani,hivyo inampasa kila
muislamu kuchukua tahadhari katika
maisha yake ya kila siku.
Mufti Menki aliongeza kuwa ili
kupata mafanikio duniani na
akhera,muislamu anapaswa kusihi kwa kutekeleza sheria za mwenyeziMungu bila ya kuchagua ikiwa ni
pamoja na kuwa mahusiano mema miongoni mwa jamii ili kuweza kuonyesha uzuri
wa uislamu.
Alisema
muislamu hapaswi kudharau dhambi yoyote kwa kufikiri
kwake kwamba dhambi fulaninindogo
kwani kila analofanywa linaandikwa na kutolea mfano wa
mwanaume anyemtazama
mwanamkebarabarani na kumsifia maumbile yake ja mbo ambalo ni makosa kwakuwa amriimekuja ya
kuinamisha macho ili usiangalie vilivyoharamishwa kwako.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa The Isalamic
Foudation yenye makao yake makuu mjini morogoro Nchini Tanzania, Al akhi, Aref
Nahdi, alisema ujio wa Mufti Menki hapa Tanzania umefungua milangoyamahusiano mema miongoni mwa waislamu katika Afrika
jambo am balo linapaswa kuenzia kwa
namna yoyote.
Aref
amesema ili kuthamini mchango wa
Mufti Menki, Taasisi ya The Islamic Foundation itaandaa mualiko maalum
kwa ma mufti kutoka Afrika ili waje Tanzania ambapo watafanyamkutano pamoja na
mufti wa tanzania lengolikiwa ni kuinyoshe jamii umoja namshikamano uliopo miongoni
mwa waislamu.
Alisema
mkutano huo utatoa fursa kwa viongozi hao wa kiislamu barani Afrika ambao wana hadhi ya Umufti, (Maprofesa)
kubadilishana mawazo na kuangalia njia sahihi za kufikisha ujumbe
ili jamii ijue kwamba uislamu sio
dini ya vurugu na badala yake kila anaetaka amani anapaswa kuchukua
mfano kutoka kwenye uislamu.
Aidha, Mwenyekiti huyo wa The Islamic Foundation Tanzania, Aref Nahdi ambae
ndie mwenyeji wa Mufti Menki, alisema anatoa shukrani kwa serikali ya
tanzania kwa kuthamini ujio wa Mufti Menki, hali iliyopelekea wepesi wa
kusafiri kati ya Dar es salaam na Morogoro.
Ameimba serikali iendelee kutoa ushirikiano kama
huo mara wageni wa kiislamu wanapoingia
hapa nchini kwani katikakujenga mahusiano mema kati ya nchi na
nchi ni
pamoja mapokezi mazuri ya kiserikali kwa wadini kutoka nje ya nchi
ambapo taasisi The Islamic Foundation i
mepanga kuwaleta viongozi kadhaa wa
kiislamu hapa nchini ambapo pamoja na kulingania katika uislamu, viongozi hao wa kigeni
pia watapata fursa ya kuchangia katika
huduma za jamii hapa nchini ikiwemo huduma za Afya,
Elimu pamoja na maji.
Mwenyekiti wa The Islamic Foundation Aref Nahdi
akiwa na Mufti Menki na
wajumbe waandamiz.
Mufti Ismail Menki, wa Zimbabwe akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili katika ofisi za The
Islamic Foundation Mjini
Morogoro nchini Tanzania, Kulia ni
Mwenyeji wake, Mwenyekiti wa
The Islamic Foundation, Aref Nahdi
Waislamu wakimsikiliza Mufti Menki, katika ukumbi
wa Diamond jublee, jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akihutubia.
No comments:
Post a Comment