Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Kamishna msaidizi wa Polisi ACP-Bonaventura Mushongi wa kwanza kushoto.
.........................................................
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MICHAEL William maarufu Michael dada ambae alikuwa akidaiwa ni mhalifu
sugu na mbakaji huko wilayani Kibaha ameuwawa na wananchi wenye hasira kali.
Michael ameuwawa huko kwenye pori la shirika la elimu
Kibaha-Tumbi,akidaiwa kuwateka watoto wa kike wawili ambao ni wanafunzi kwa
lengo la kuwabaka.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani,Bonaventura Mushongi akizungumzia tukio
hilo,alisema watu hao walimshambulia mtu huyo sehemu mbalimbali za mwili na
kumsababishia kifo.
Kwa mujibu wa kamanda huyo wa polisi,alisema tukio lilitokea juzi saa 10
alasiri.
Alisema marehemu huyo alimchukua mwanafunzi mwenye umri wa miaka (11)
anaesoma shule ya msingi Kibaha na mwingine mwenye miaka (6) mwanafunzi wa
shule ya chekechea ya mama Kawili wote wanaishi Picha ya Ndege.
“Watoto hao walikuwa wakicheza rede
mtaani kwao karibu na baa ya Lekashingo kata ya Picha ya Ndege ambapo Michael
aliwashawishi wamsindikize mtaa wa Lulanzi kwenda kuchukua mzigo wake ambao
aliusahau”
“Watoto hao walimkubalia na
kuanza kuongozana nae lakini wakiwa njiani ghafla lilitokea gari aina ya toyota
noah nyeusi ambayo haikuweza kufahamika namba zake za usajili na kuondoka nao
kwenda nao pori la shirika la slimu Kibaha karibu na shule ya sekondari ya
Tumbi’
“Wakiwa katika pori hilo mtoto
mkubwa alimponyoka wakiwa wamefika kwenye bwawa la maji machafu kisha kuomba
msaada ndipo kundi la watu lilipojitokeza na kuanza kumkimbiza na walipomkamata
walimpiga hadi kufariki dunia,” alisema kamanda Mushongi.
Kamanda Mushongi ,alisema uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi
umebaini marehemu alikuwa mhalifu mzoefu na alikuwa akifanya matukio ya mara
kwa mara ikiwemo ya ubakaji na wizi wa mifugo.
Alisema hivi karibuni alikamatwa na kufikishwa mahakama ya wilaya ya
Kibaha kwa kosa la kuiba ngombe wanne.
Michael aliachiwa huru yeye na mwenzake Said Mohamed baada ya mlalamikaji
kushindwa kufika mahakamani baada ya kuwapata ngombe wake kwa kesi
iliyofunguliwa namba KBH/STPU/02/2014.
Jeshi hilo limewakemea wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi badala
yake wawafikishe watuhumiwa kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment