Muonekano
wa Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa Afya na kutoa huduma ya Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) iliyopo
eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Hospitali hiyo
hiyo ya kisasa inatarajiwa kufunguliwa rasmi Januari Mwakani.
Daktari
Bingwa wa Uchunguzi wa mionzi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dr Lulu Fundikira akiwaonyesha waandishi wa habari
wa vyombo mbalimbali mashine ya CT-Scan iliyopo kwenye Hospitali ya
Kisasa ya kufundishia wataalamu wa Afya na kutoa huduma iliyopo eneo la
Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakati waandishi hao
walipotembelea hospitali hiyo jana. Hospitali hiyo hiyo ya kisasa inatarajiwa
kufunguliwa rasmi Januari Mwakani.
Daktari
Bingwa Wa tiba za dharura kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dr Andrew Sawe akiwaonyesha waandishi wa habari wa
vyombo mbalimbali vitanda vya kisasa kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji
uangalizi maalumu viliyopo kwenye Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu
wa Afya na kutoa huduma iliyopo eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la
Dar es Salaam wakati waandishi hao walipotembelea hospitali hiyo jana.
Hospitali hiyo hiyo ya kisasa inatarajiwa kufunguliwa rasmi Januari Mwakani.
....................................
Hospitali ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
, iliyojengwa kisasa kwa kutumia mifumo mbalimbali ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA, itakuwa ya kwanza kutumia mfumo wa teknolojia ya sampuli
hewa, unaochukua vipimo kwa mtambo maalum na kuwasilisha majibu kwa njia ya
mtandao.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara maalum katika jengo hilo
lililokamilika ujenzi wake rasmi tangu Agosti, mwaka huu, Makamu Mkuu wa chuo
cha MUHAS, Profesa Ephata Kaaya, alisema hospitali hiyo, itatoa tiba ya
magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa sugu kama vile, moyo, saratani na figo.
Hospitali hii ni ya kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na
kutoa huduma ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
iliyopo eneo la kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam, inatarajiwa
kufunguliwa na kuanza kutoa huduma Januari mwakani.
Hospitali hiyo, imejengwa na kufungwa vifaa tiba vya kisasa vya digitali,
vinavyotumia zaidi teknolojia ya Tehama zikiwemo mashine za X-ray, MRI,
CT-Scan, mashine maalum kwa ajili ya kupimia magonjwa ya wanawake, mashine
maalum za kupima na kutibu meno, koo, masikio na pua.
“Pia umefungwa mtambo wa kisasa zaidi wa sampuli hewa uliopo katika kila
idara na kuunganishwa na maabara ambao kazi yake ni kusafirisha vipimo na
kupeleka sehemu mbalimbali na majibu ya vipimo hivyo huwasilishwa sehemu husika
kwa njia ya mtandao,” alisema.
Alisema mtambo huo, unasaidia kupunguza tatizo la msongamano katika
chumba cha maabara, unaongeza ufanisi na usahihi wa vipimo lakini pia hupunguza
muda na kuepusha mkanganyiko wa vipimo.
Hospitali hiyo pia itatoa huduma za kufundishia, kufanya uchunguzi
wa magonjwa mbalimbali na tafiti za fani za afya. “Lakini pia tuna vyumba
maalum 12 kwa ajili ya wagonjwa wenye magonjwa ambukizi kama vile ebola,
kipindupindu na kifua kikuu.
Profesa Kaaya, amesema ujenzi wa hospitali hiyo uliogharimu kiasi cha
dola za Marekani milioni 94.5 katika eneo hilo la Mloganzila lenye ukubwa wa
ekari 3,800, ulianza tangu mwaka 2014 kupitia mkopo wenye riba nafuu ambao
malipo yake yataanza kulipwa baada ya miaka 15 kwa kipindi cha miaka 25.
Amesema jengo la hospitali hiyo lina ghorofa tisa ambazo zinajumuisha
vyumba 13 vya upasuaji kikiwemo chumba kimoja cha upasuaji kwa wagonjwa wa
dharura, wodi za watoto, maabara za kisasa, vyumba vya wagonjwa mahtuti na
kusafisha figo, wodi za kujifungulia, chumba cha kuhifadhia maiti na vyumba vya
kufundishia.
Aidha amesema katika eneo la wodi zipo wodi 12 za wagonjwa mashuhuri
vikiwemo vyumba viwili vyemye mitambo ya kisasa ya kufuatilia hali ya mgonjwa
vya viongozi wenye hadhi ya juu ikiwemo Rais.
Daktari
Bingwa wa koo, Masikio na Pua kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dr Daudi Ntunaguzi akiwaonyesha waandishi wa
habari wa vyombo mbalimbali utendaji kazi wa moja ya kifaa cha kisasa cha
kuchunguza masikio kilichopo kwenye Hospitali ya Kisasa ya kufundishia
wataalamu wa Afya na kutoa huduma iliyopo eneo la Mloganzila nje kidogo
ya jiji la Dar es Salaam wakati waandishi hao walipotembelea hospitali hiyo
jana. Hospitali hiyo hiyo ya kisasa inatarajiwa kufunguliwa rasmi Januari
Mwakani.
Baadhi
ya madaktari bingwa na wataalamu mbalimbali wakisikiliza maelezo ya wataalamu
wa ujenzi wa jengo hilo yaliyowasilishwa leo mbele ya waandishi wa habari.
Juma
Bernard Mkuu wa Kitengo cha Mfumo wa Mawasiliano MUHAS Academic Medacal Centre
Mloganzila akifafanua jambo katika maelezo kwa waandishi wa habari wakati
alipotembelea hospitali hiyo.
Profesa
Ephata Kaaya akizungumza na waandishi wa habari na kuwaelezea juu ya
mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS
iliyopo eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es
Salaam , Kulia ni Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Said Aboud.
Omari
Kileo Mhandisi wa Umeme MUHAS Academic Medacal Centre Mloganzila
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati alipotembelea na kujionea
ujenzi wa chuo hicho.
Andrew
Fungamali akielezea jinsi mfumoa wa maji safi na maji taka unavyofanya
kazi katika chuo hicho.
Andrew
Fungamali akielezea na kuonyesha jiko kwa ajili ya kupikia chakula cha wagonjwa
katika chuo hicho.
No comments:
Post a Comment