Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akihutubia Mkutano
wa 17 wa Dhara\ula wa Nchi za Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa
Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016
................................
RAIS John
Pombe Magufuli amewataka Viongozi na wananchi wa Sudan Kusini kutanguliza
mbele maslahi ya nchi yao ili kusaidia kumaliza mgogoro wa kisiasa unaondelea
nchini humo.
Akizungumza
katika mkutano wa 17 wa Jumuiya hiyo leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa
Jumuiya hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli alisema jumuiya hiyo inasikitishwa na mapigano ya ghafla yaliyoibuka
hivi karibuni nchini humo.
Rais Magufuli
suala la amani na usalama ni jambo umuhimu si kwa ustawi wa maendeleo ya taifa
hilo pekee bali pia kwa mustakabali wa mataifa mengine yaliyopo ndani ya
jumuiya hiyo.
Aidha Rais
Magufuli aliipongeza Jumuiya ya Ushirikiano wa Kieneo ya Mashariki mwa Afrika
(IGAD) inayoundwa na nchi za Eritrea, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na
Uganda katika jitihada zake kusuruhisha mgogoro huo.
Aidha Rais
aliipongeza nchi ya Sudan Kusini kuwa mwanachama kamili wa Jumuiya hiyo na
kuwahakikishia kuwa jumuiya hiyo itatoa ushirikiano wa kutosha katika
kuhakikisha ikuwa nchi inapata amani ya kudumu ili wananchi wake washiriki
katika shughuli za maendeleo.
“Sekretarieti
ya jumuiya hiyo inaendelea na maandalizi ya kujumuisha nchi ya Sudan Kusini
katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na nchi wanachama” alisema
Rais Magufuli.
Kwa upande
wake, mwakilishi maalum wa Rais wa Sudan Kusini, Aggrey Tisa Sabuni aliishukuru
jumuiya hiyo kwa uamuzi wa kuikubali nchi hiyo kuwa mwanachama mpya wa jumuiya
hiyo na kuwakikishia kuwa taifa hilo litarejeshea hali ya utulivu na usalama.
“Jaribio la
mapinduzi la mwezi julai mwaka huu limeleta athari kubwa kwa wananchi wetu,
hata hivyo tunawahakikishia kuwa tutakuwa mshirika wa kweli wa jumuiya hii”
alisema Sabuni.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Naibu
Rais wa Kenya Mhe William Rutto baada ya Mkutano wa 17 wa Dharula
wa Nchi za Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam
leo Septemba 8, 2016.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli na viongozi wenzie wakisimama
wakati wimbo wa Jumuiya ukipigwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Dharula
wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu
jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli na viongozi
wenzie wakiendelea na Mkutano wa 17 wa Dhraula wa Nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo
Septemba 8, 2016
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya
pamoja na viongozi wenzie baada ya Mkutano wa 17 wa Dharula wa Nchi
za Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo
Septemba 8, 2016
No comments:
Post a Comment