Mkuu
wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi.
......................................
Ulaji wa vyakula visivyo bora husababisha maradhi ya magonjwa ya moyo kwa
watu wazima wa miaka 45 hadi 60 huku watoto wadogo pia wamegundulika kuwa ni miongoni mwa waathirika
wa ugonjwa wa moyo, wanaoupata kutokana na kurithi kutoka kwa wazazi wao.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Msemaji Mkuu wa
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Bw. Maulid Kikondo wakati wa maadhimisho ya
siku ya moyo duniani ambapo kitaifa ilifanyika katika taasisi hiyo.
Kikondo alisema kuwa katika kuadhimisha siku hiyo Taasisi hiyo imeamua
kupima wagonjwa wa moyo bure ili kuwasaidia wananchi kuweza kufahamu njia
bora za kuweka kukabiliana na magonjwa hayo.
Kikondo alisema kuwa wazee na watoto hupata maradhi ya moyo kwa wingi
nchini kutokana kula vyakula visivyo na mpangilio pamoja na kukosa kufanya
mazoezi kwa muda mrefu.
“Ugonjwa wa moyo huwapata zaidi
watoto kutokana kwa kurithi au kutopata mlo ulio bora na mpangilio wakati wazee
hupata ugonjwa huu kutokana na msongo wa mawazo pamoja na kutofanya mazoezi
mara kwa mara hivyo kupelekea kupata presha na mwisho wake ni ugonjwa wa moyo” alisema Kikondo.
Aidha Kikondo alisema kuwa wagonjwa wa moyo wanaopatikana kwa siku ni
kuanzia wagonjwa 200 na kuendelea kiasi ambacho ni hatari kwa maendeleo ya nchi
hasa kwa taifa linaloelekea katika uchumi wa kati.
Kwa upande wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo
Dkt. Delilah Kimambo imesema kuwa inasadikika duniani kote kati ya watu milioni
17.3 hupoteza maisha yao kutokana na ugonjwa wa moyo.
Siku ya Moyo Duniani huadhimishwa Septemba 29 kila mwaka ili kuhamasisha
watu kuhusu afya ya Moyo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “YAPE NGUVU MAISHA
YAKO”.
No comments:
Post a Comment