Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha ziara ya siku tatu nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa ahudhurie sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe.Edgar Chagwa Lungu ili aweze kushughulikia tatizo la tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16 ,mamia wakiwa wamejeruhiwa na nyumba kadhaa kubomolewa mkoani Kagera.
Kufuatia kuahirisha ziara hiyo Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumuwakilisha katika sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa LunguRais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zinatarajiwa kufanyika keshokutwa tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.
Jaffar HaniuMwandishi wa Habari wa Rais MsaidiziDar Es Salaam11 Septemba, 2016

No comments:
Post a Comment