Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia aliposimama
Nangurukuru, wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wakati akiwa njiani kuelekea
mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.
mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.
Sehemu
ya Wakazi wa Nangurukuru mkoani Lindi wakishangilia ujio wa Makamu wa Rais Mhe.
Samia Suluhu Hassan.
Makamu
wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi katika mji wa
Nangurukuru Wilaya ya Kilwa waliojitokeza kwa wingi wakati akipita kuelekea Mkoani
Mtwara kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
Makamu
wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi alipokuwa
akiwasalimia wananchi katika mji wa Nangurukuru Wilaya ya Kilwa
waliojitokeza kwa wingi wakati akipita kuelekea Mkoani Mtwara
Baadhi
ya wananchi aliojitokeza kumlaki Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu wakati
akipita kwenye mji wa Nangurukuru wilayani Kilwa.
.........................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itatuma kikosi
maalum cha kukabiliana na uvuvi haramu unaoendelea katika bahari ili kudhibiti tatizo hilo ambalo limeathiri sana mazalia ya samaki na kuchangia kupungua kwa samaki baharini.
Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 7-Sept-2016 wakati akisalimiana na wananchi wa
Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi ambao walijitokeza kumsalimia wakati
akielekea mkoani Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku NNE mkoani huo.
Makamu wa Rais amesema
katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika vizuri serikali pia itatuma wataalamu
wa mazingira ambao watafanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika bahari
ili kujua uharibifu uliofanyika na kuchukua hatua ya kukabiliana na hali hiyo.
Ameeleza kuwa serikali
itachukua hatua hizo ili kuinusuru bahari kwa sababu imekuwa ni chanzo kizuri
ya mapato kwa wananchi kutokana na shughuli za uvuvi na shughuli nyingine
zikiwemo za utalii.
“Bahari yetu ndio mapato
yetu, bahari yetu ndio maisha yetu tumeitumia vibaya mapato yamepungua na
maisha hayawi mazuri hivyo ni muhimu tuitunze ili iendelee kutulea kwa manufaa
mazuri.”
Kuhusu uboreshaji wa
huduma za afya kwa wananchi wa Kilwa, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti zinazolenga kuhakikisha
wananchi wote nchini wanapata huduma bora za afya katika ngazi zote.
Amesema mpango huo wa
uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi nchini utaenda pamoja na utoaji wa
elimu bora wa wanafunzi kote nchini chini ya mkakati wa serikali wa kutoa elimu
bure kuanzia wanafunzi darasa la kwanza hadi kidato cha nne.
Katika ziara yake mkoani
Mtwara, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
kesho 8-Sep-16 atazindua jengo la ofisi za Tume ya Maadili ya Uongozi wa
Umma Kanda ya Kusini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Makamu wa
Rais tayari amewasili mkoani Mtwara na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa
mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego pamoja na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela
Kairuki.
No comments:
Post a Comment