Mkuu wa wilaya ya Bukoba Mh. Deodatus Kinawiro amethibitisha kufariki kwa
watu 11 na wengine 196 kujeruhiwa katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera
kufuatia tetememko la ardhi lenye ukubwa wa vipimo vya 5.7 lililotokea mkoani
humo na kusababisha madhara makubwa.
Alisema tetemeko lililotokea mchana wa jana jumamosi tarehe 10
septemba 2016 lilikuwa ni kubwa na limeathiri majengo mengi na kusababisha
majeruhi na vifo.
Hata hivyo bado Kamati ya Ulinzi na Usalama ikishirikiana na vikosi vya
uokoaji pamoja na majeshi la ulinzi na usalama vinaendelea kufanya tathmini ya
uharibifu wa majengo na mali uliosababishwa na Tetemeko hilo.
DC Kinawiro ameongeza kwamba taarifa zaidi zitaendeleo kutolewa kadri
zitakavyopatikana kutokana na kuendelea kwa kazi ya tathmini ya
athari ya tetemeko hilo.
No comments:
Post a Comment