Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akisalimiana
na Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzania na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe
(MB) wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akijibu
maswali ya wabunge wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania leo Mjini Dodoma.
Kiongozi
wa Kambi rasmi ya Upinzania na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe (MB) akimuuliza
swali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB)
kuhusu hali ya uchumi nchini ambapo Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa alimhakikishia
kuwa Serikali ipo imara katika kusimamia ipasavyo uchumi wa nchi.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akiwashukuru
wabunge mara baada ya kumaliza kujibu maswali wakati wa kikao cha tatu cha
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini Dodoma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) akijibu swali bungeni ambapo
alisema kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na raia katika kuhakikisha
inakabiliana na biashara haramu ya Madawa ya Kulevya.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan
Kolimba akijibu swali bungeni ambapo alisema serikali ipo katika mazungumzo na
serikali ya China kwa ajili ya kuboresha zao la Tumbaku.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akijibu swali
bungeni ambapo alisema Wizara imetenga Shilingi bilioni 3 kwa ajili ya
kuboresha hali ya Magereza nchini.
Waziri
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akijibu swali bungeni ambapo alisema ambapo alisema Serikali
imetenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kuboresha Magereza ya watoto
pamoja na makao ya Wazee nchini.
Spika
wa Bunge Mh. Job Ndugai akitoa mwongozo katika moja ya mambo wakati kikoa cha
bunge kikiendelea mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment