Mkuu
wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa wakati Muhimbili (MNH), Dk Flora
Lwakatare akieleza jambo kwa waandishi wa habari leo.
Mkuu
wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo akizungumza na waandishi wa habari leo
baada ya mashine ya MRI kuanza kufanya kazi. Kutoka kulia ni Mtaalamu wa MRI
(MRI Technologist), Joshua Job na Daktari Bingwa wa Mionzi, Mussa Ndukeki wa
hospitali hiyo.
Waandishi
wa habari wakiwa katika mkutano uliofanyika leo kwenye hospitali hiyo.
Mtaalamu
wa MRI (MRI Technologist), Medadi Mallaya akimuhudumia mgonjwa leo.
..............................................
Mashine ya MRI katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) imepona baada ya kuharibiika tarehe 24/08/2016. Mashine hiyo
iliharibiika baada ya kutokea hitilafu ya umeme.
Tangu mashine hiyo imepona tayari wagonjwa 52 wamepatiwa kipimo cha MRI.
Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare amesema baada ya mashine hiyo
kuharibiika, mafundi wa Philips kwa kushirikiana na mafundi wa Muhimbili walibadilisha
betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hiyo.
“Tarehe 26/08/2016, mafundi
walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine
hii kwa kuwa betri za awali zilikuwa zimefungwa muda mrefu. Tarehe 28/08/2016
mafundi walibaini kwamba kifaa cha Gradient Module kilikuwa kimeharibiika na
tayari hospitali kwa kushirikiana na Philips wameagiza kifaa hicho kutoka
Uholanzi,” amesema Dk
Lwakatare.
Mmoja wa ndugu wa wagonjwa, Lazaro James, mkazi wa Singida amesema kwamba
tangu kuharibiika kwa mashine ya MRI alikuwa akiisubiri na kwamba amefurahi
baada ya kurejea kwa huduma hiyo.
“Tunashukuru huduma za MRI zimerejea hapa Muhimbili, gharama zake ni
nafuu kuliko kuliko kupata matibabu nje. Jambo lingine napenda kuwapongeza
madaktari na wauguzi kwa utendaji bora.
Naye Hawa Hussein mkazi wa jijini Dar es Salaam, ameishukuru Hospitali ya
Taifa Muhimbili kwa kuwa imekuwa ikitoa huduma bora kwa wagonjwa.
Hawa ameuopongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kufanya juhudi za
kuiwezesha mashine hiyo kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa.
Alisema kwamba madaktari wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii hivyo wana
imani wataendelea kupata huduma bora na kwa wakati.
No comments:
Post a Comment