Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiingia kwenye uwanja wa michezo wa
Kibiti wilayani Kibiti ambapo Waziri Mkuu alihutubia mkutano wa hadhara ,
Septemba 26, 2016. . Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest
Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akimshukuru Mzee Abadallah Ngwele baada ya kupokea
madawati 10 yaliyotolewa na wazee wa Kibiti katika mkutano wa hadhara
aliouhutubia kwenye uwanja wa michezo wa Kibiti, Septemba 26, 2016.
Kushoto ni mkewe Mary na watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi
Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
...................................
WAZIRI MKUUkuu ,Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Afisa Elimu Mkoa wa
Pwani, Yussuph Kipengele kupeleka walimu wa kufundisha masomo ya kidato cha
tano na sita katika shule za sekondari za Mkongo na Utete wilayani Rufiji.
Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza na
wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la
Maendeleo wilayani Rufiji.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Rufiji, Muhammed
Mchengelwa kumwambia kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa
walimu wa kidato cha tano na sita licha ya kuwa na shule.
“Hatuwezi kuwa na shule ambazo hazina walimu, nasikia hapa anayefundisha
ni Mkuu wa shule na mwalimu mmoja tu, wakati kule Kibaha kuna walimu
walmerundikana ,sasa fanya realocation tarehe 4,Oktoba uniletee taarifa walimu
wamefika Rufiji.”,alisema Waziri Mkuu.
Akizungumzia suala la upungufu wa watumishi wa umma kwenye sekta
mbalimbali, Waziri Mkuu alisema baada ya kazi ya uhakiki watumishi hewa
itakapokamilika, serikali itaangalia kwenye maeneo yenye upungufu na hivyo
kutangaza ajira.
“Hivi sasa serikali inakamilisha masuala ya uhakiki wa watumishi,
tukimakamilisha na kujua idadi ya watumishi na maeneo yenye upungufu tutaanza
tena kuajiri, tulisitisha kupisha kwanza kazi hii,alisema Waziri Majaliwa.
Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji Waziri, Mkuu alisema
watendaji wa halmashauri na vijiji wanapaswa kutenga maeneo ya wafugaji na
wakulima na kutaka mifugo isiongezwe kwenye maeneo ambayo hayajaruhusiwa.
Alisema wenyeviti wa vijiji wanapaswa kusimamia utekelezaji wake katika
mpango wa matumizi bora ya ardhi na kwamba atakayeruhusu idadi kubwa ya mifugo
kuingia kijijini zaidi ya ile iliyokubalika atawajibishwa ikiwemo kufukuzwa
kazi na hatua nyingine za kisheria.
“Hatuwezi kuendelea kuwa na watumishi wasio na nidhamu, wale wote
watakaoingia mifugo zaidi ya uwezo wa kijiji wafukuzwe kazi na kuchukuliwa
hatua, lakini pia wafugaji ni marufuko kuingiza mifugo kwenye mazao ya
wakulima”alisema Waziri Mkuu.
Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kwenda makao makuu ya wilaya ya Rufiji,
Utete, Waziri Mkuu aliahidi kuchukua ombi hilo na kusema bajeti ijayo
litatengewa fedha kuwa ajili ya kufanya maandalizi ya upembuzi kuona gharama
yake kabla ya kutangaza zabuni ya ujenzi.
Kuhusu utengenezaji wa madawati, Waziri Mkuu alisema ifikapo Oktoba 30,
mwaka huu kila wilaya nchini inapaswa iwe imekamilisha utengenezaji wa madawati
hayo kwenye shule nchini.
Aidha, alisema ipo miradi mingi inayoendeshwa kwa maslahi binafsi ukiwemo
mradi wa Bonde la Rufiji(RUBADA), ambao wamebaini kuna ubabaishaji mkubwa,
hivyo wamepeleka timu ya wataalamu kuhakiki ili wale wabadhirifu wachukuliwe
hatua.
No comments:
Post a Comment