Makamo wa Rais,
Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa
umma kanda ya kusini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa halfa fupi ya
uzinduzi wa jengo la
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara
..........................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma Nchi kuchunguza na kuwachukulia hatua kisheria na za
kinidhamu viongozi na watumishi wa umma ambao wanakiuka taratibu za kazi kwa
ajili ya maslahi yao binafsi.
Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 8-Sep-2016 mjini Mtwara wakati anafungua jengo
la sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini ambalo ujenzi
wake umegharimu takribani shilingi Bilioni mbili.
Makamu wa Rais amesema
iwapo kama hatua hizo zitachukuliwa haraka zitakomesha na kupunguza kasi ya
mmomonyoko wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma hali ambayo itaongeza
uwajibikaji katika utendaji wa kazi miongoni watendaji hao.
Amesisitiza kuwa serikali
itaendelea kuiimarisha sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma nchini kwa
kuijengea uwezo wa rasilimali watu na fedha kwa kadri hali ya uchumi itakavyo
ruhusu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Makamu wa Rais
amewahimiza viongozi na watumishi wa umma kuthamini na wahakikishe walinda
maslahi ya umma wakati wote wa utendaji wao wa kazi ili kuondoa malalamiko kwa
wananchi.
Makamu wa Rais amesema ni
jambo la muhimu kwa sekretarieti hiyo kufutilia mienendo ya viongozi wa umma na
kuwabaini wale wanaokwenda kinyume na misingi ya uadilifu na wachukuliwe hatua
ipasavyo kabla hawaleta madhara kwa serikali na jamii kwa ujumla.
Makamu wa Rais pia ametoa
rai maalum kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara kuitumia ofisi hiyo mpya ya
sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini kwa kutoa taarifa
kuhusu mienendo ya viongozi wanaokiuka maadili ya umma katika utendaji wao wa
kazi ili waweze kuchukuliwa hatua.
Kwa upande wake Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela
Kairuki amessitiza kuwa kazi ya kuhakiki mali na madeni ya viongozi wa umma
itaendelea kwa kasi nchini na mwaka huu sekretarieti hiyo itahakiki mali za
viongozi wapatao 500 kote nchini.
Naye Jaji Mstaafu na
Kamishna wa Maadili Nchini Salome Kaganda akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo
hilo ameiomba serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kufanikisha zoezi
la uhakiki wa mali na madeni ya viongozi kwa nchi nzima.
Jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara
Kamishna wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili
ya Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akihutubia kwenye hafla hiyo
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais
Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akihutubia
kwenye hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment