Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira,
akizungumza na wakuu wa Idara na vitengo vilivyopo chini ya wizara
wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya kiutendaji katika wizara
hiyo.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.Mkutano huo umefanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Wakuu
wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, wakati wa mkutano
wa kujadili masuala ya kiutendaji katika wizara hiyo. Mkutano huo
umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi
kutoka Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani, kutoka kulia ni Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Magereza, John Minja, Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, Rogasius Kipali na Kamishna wa Fedha Jeshi la Polisi, Albert
Nyamhanga, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara, Meja Jenerali Projest
Rwegasira(hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya kiutendaji
katika wizara hiyo. Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment