Sunday, September 18, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI, APOKEA MSAADA WA DOLA 200,000 KUTOKA KWA RAIS WA UGANDA KUSAIDIA WAHNGA WAHANGA WA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA.

bub1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha kiasi cha  dola laki mbili (USD 200,000) kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha wapili kutoka (kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera.bub5

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  mchango wa fedha kiasi cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam.bub7

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha mara baada ya kuwasilisha mchango wa kiasi cha fedha Dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.bub8

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Boniface Muhia mara baada ya kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kwa misaada mbalimbali ambayo inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka Kenya muda wowote. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment