Monday, September 12, 2016

SWALA YA EID BAGAMOYO, ILIYOSWALIWA BONG'WA.

Waislamu mjini Bagamoyo, wakiswali swala eid katika viwanja vya  Istqaama  leo.

Waislamu wilayani Bagamoyo wametakiwa kusherehekea siku kuu yaEidi kwa utulivu na amani huku wakizingatia mafundisho ya  mtume Muhammad Swalallaahu Alayhi wa Salaam.

Wito huo umetolewa na katibu wa baraza la Ulamaa la Taasisi ya SirajulMunir Islamic Cente (SIMIC) ya mjini Bagamoyo, alipokuwa akitoa  hutuba ya swala yaeidi iliyoswaliwa  katika  viwanja vya  masjidi Istiqaama eneo la Bong'wa Bagamoyo mjini.

Alisema uislamu umefundisha  m ichezo mbalimbali, hivyo ni vyema  katika ya sikukuu waislamu wakifanya  michezo mbalimbali iliyoruhusiwa katika uislamu.

Aliongeza  kwa  kuwataka wazazi wawape watoto mafundisho ya namna ya  kufurahi katika siku kuu ili kuepuka katika kufanya  mambo yanayokwenda kinyume na uislamu ikiwa ni  pamoja na aina gani yamavazi yanayopaswa  kwa  watoto pamoja  sehemu zinazofaa kwa  watoto kutembelea.

Alisema  katika sikukuu hii waislamu wanakumbuka historia ya nabii Ibrahim  ambae  alionyesha umahiri m kubwa katika kumtii mwenyeziMungu yeye na familia yake, hali iliyopelekea kutii  amri hata ya  kumchinja  mwanae.

Aliendelea kusema  kuwa, uislamu katika kugawa haki na majuku kwa watu umezingatia uadilifu na sio usawa ieleweke kwamba  katika uislamu uadilifu umepewa umuhimu wake na hii ni  pamoja na kufuata  sheria zote za  mwenyezimungu.

Waislamu wa Bagamoyo na Tanzania kwa ujumla leo wanaungana na waislamu duniani kote kushereheka siku kuu ya  kuchinja ambayo inaadhimishwa mara baada ya kukamilisha ibada ya hija ambayo ni nguzo ya tano katika uislau inayotekelezwa  kila mwaka huku Maka SaudiArabia.




No comments:

Post a Comment