WAZIRI MAKAMBA AITAKA NEMC KUIGA UTENDAJI WA TFS

Image may contain: 4 people, people standing and suit
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira ) Mhe. January Makamba (kushoto) akimkabidhi rasmi vitendea kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo mara baada ya kuzindua Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.



Prof. Silayo ni miongoni mwa wajumbe nane walioteuliwa kuunda bodi ya NEMC itakayohudumu kwa kipindi cha miaka mitatu ikiwa chini ya mwenyekiti wake, Dkt. Flora Ismail Tibazwara.


Akiwakabidhi vitendea kazi (Sheria, Kanuni na Sera ya Mazingira) hivyo Mhe. Makamba aliitaka bodi hiyo kufanya mapinduzi ya kiutendaji kwa kuiga mfano wa TFS iliyoko katika wilaya zote nchini.


“Naamini mambo yatakwenda kubadirika sasa, NEMC kwa sasa inafanya kazi ya kutoa vyeti tu, sisemi hawafanyi kazi la hasha, wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanasimamia sheria, kanuni na taratibu lakini hawajajipambanua hivyo, sasa ibadirisheni NEMC iwe kama TFS, wao wapo kila wilaya hata kusiko na misitu, wapo kuhakikisha wanasimamia sheria, kanuni na taratibu; katika hili msiwe na shaka Serikali iko nyuma yenu” aliwasisitiza wajumbe wa bodi Mhe. Makamba.


Wajumbe wengine wanaounda Bbdi hiyo ni Prof. Hussen Sosovela, Dkt. Catherine Masao, Damas Masolongo, Dkt. Neduvoto Mollel, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa na Prof. William Mwigoha

Comments

Popular posts from this blog

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.