NA MWAMVUA MWINYI,
PWANI
MAKOSA ya ubakaji
yametajwa kuongezeka kutoka 206 kwa mwaka 2017 na kufikia 271 mwaka 2018, mkoani
Pwani .
Aidha kupatikana na silaha
mwaka 2017 yalikuwa makosa tisa ambapo mwaka uliopita 2018, yameongezeka na
kufikia 26 .
Akielezea tathmini ya hali
ya uhalifu katika kipindi cha mwaka 2018 ikilinganisha na mwaka 2017, kamanda
wa polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Wankyo Nyigesa
alisema tathmini ya kijumla inaonyesha wamepunguza matukio 151 makubwa .
Alisema, makosa ya ubakaji
yameonekana kupanda kutokana na uelewa kwa jamii na mwamko wa kuripoti matukio
hayo polisi.
Wankyo alieleza, matukio
ya mauaji yalikuwa 61 ikilinganisha na matukio 70 yaliyoripotiwa mwaka 2017 .
“Makosa ya kufanya
biashara ya kusafirisha binadamu mwaka 2018, yalikuwa 03 ikilinganishwa na
makosa 05 yaliyorekodiwa mwaka 2017″alifafanua Wankyo.
Kamanda huyo alisema kuwa,
makosa ya unyang ‘anyi wa kutumia silaha mwaka 2017 yalikuwa 21 na mwaka 2018
makosa hayo ni 13.
Unyang’anyi wa kutumia
nguvu mwaka 2017 yaliriporiwa makosa 126 ,wakati mwaka 2018 makosa ya namna
hiyo yameripotiwa makosa 52 .
Alisema, jeshi hilo pia
limefanikiwa kudhibiti uingizaji bidhaa kupitia bandari bubu wilayani Bagamoyo
kwa kukamata makosa 27,watuhumiwa 31 pamoja na madumu 5,435 ya mafuta ya kula
aina mbalimbali .
“Sukari kutoka nchi za nje mifuko 78, mabello 20
ya nguo za mitumba aina mbalimbali ikiwemo manne ya khanga na vyombo vya moto
vilikamatwa ikiwa ni pamoja na pikipiki sita na magari matatu. “alieleza
Wankyo.
No comments:
Post a Comment