Na Omary Mngindo, Kisarawe
JUKWAA
la Wazalendo wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani, Jumamosi ya Jan 13 limekabidhi
Mashine ya Kudurufu moja sanjali na Kompyuta vyenye thamani ya sh. Mil. 6.
Vifaa
hivyo vinavyolenga kutumika kuchapishia mithihani kwenye shule za sekondari na
msingi zilizomo Tarafa ya Marumbo, lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanapata
fursa nzuri ya kushiriki masomo, yatayowawezesha kufanya vizuri kwenye
mithihani yao.
Katika
hafla hiyo iliyoambatana na Mkutano Mkuu wa mwaka kwa wana-Jukwaa hilo,
uliofanyika Kijiji cha Malumbo Kata ya Mfulu Tarafa ya Manerumango wilayani
hapa, umehudhuliwa na mamia ya wana- Kisarawe, wakiongozwa na mgeni rasmi
Mhandisi Wakati Mwaruka.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Mhandisi Mwaruko alisema kuwa lengo la
kukabishi vifaa ni kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa wilaya humo, inayolenga
kutokomeza ziro ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali wilayani humo
inayodhamilia kuinua kiwango cha elimu.
"Jukwaa
la Wazalendo linaundwa na wana- Kisarawe na wapenda maendeleo wengine kutoka
maeneo mbalinbali hapa nchini ambai kwa umoja wetu tumeanzisha Group la
Wazalendo Kisarawe, ambao kwa umoja wetu tunajitoa katika shughuli za
kimaendeleo, ikiweno shida mbalimbali kwa wana-Jukwaa," alisema Mhandisi
Mwaruko.
Mwaruko
alisema kwamba vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa shule ya Sekondari ya Kibuta na
ya msingi Mfuru, vinalenga kuwapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu, kwenda
kupata huduma ya kuchapa mitihani yao, hali ambayo kwa namna moja au nyingine
ilikuwa inachangia kukwamisha juhudi za upatikanaji wa elimu.
Akitoa
neno la kushukuru kwa wana-Jukwaa la Wazalendo Kisarawe, Afisa elimu Kata ya
Marumbo, Harrison Ukwai alisema kwamba msaada huo utasaidia kuboresha mazingira
ya utoaji elimu kwenye Kata hizo na kuongeza ufaulu.
"Msaada
huu ni mkubwa, wana-Jukwaa wameonesha ni namna gani wanavyogushwa na changamoto
nyingi ikiwemo ya elimu, ambayo kimsingi ndio sekta muhimu inayozalisha
viongozi katika maeneo yote hapa nchini na duniani kwa ujumla," alisema
Ukwai.
No comments:
Post a Comment