Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akizungumza alipowasili ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Geita alipofanya ziara katika mkoa huo jana kufuatilia utekelezaji wa
maagizo yake kuhusiana na sekta ya ardhi katika halmashauri za Mji na Wilaya ya
Geita.
........................................
Na Munir Shemweta, WANMM
Geita.
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amekerwa na makusanyo madogo
ya mapato katika halmashauri mbalimbali nchini kupitia kodi ya ardhi.
Akizungumza na watendaji
wa sekta ya ardhi wa Halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita jana mkoani Geita
alipofanya ziara ya kushtukiza kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa
katika halmashauri hizo, Dk Mabula alisema, mapato ya sekta ya ardhi katika
halmashauri nyingi hayaridhishi na kueleza kuwa halmashauri nyingi mapato yake
yako chini ya asilimia 30.
Alisema pamoja na
halmashauri hizo kuwa na mapato kidogo kupitia sekta ya ardhi lakini watendaji
wake hawaoneshi jitihada zozote kuhakikisha wanakusanya mapato ya kutosha
kupitia sekta hiyo na hivyo aliwataka watendaji hao kuongeza kasi ya ukusanyaji
mapato kwa kuwa msisitizo wa serikali ya awamu ya tano ni kukusanya kodi.
‘’Kwa staili hii tutafika
kweli? Mna bahati mbaya sasa watendaji wa sekta ya ardhi katika halmshauri
mtakuwa chini ya wizara moja kwa moja na rais amepiga kelele kuhuisiana na kodi
ninyi mnarelax’’ alisema Dk mabula.
Hata hivyo, Dk Mabula
aliisifu halmashauri ya Mji wa Geita kwa kukusanya mapato kwa zaidi ya asilimia
sitini. Kwa Mujibu wa taarifa ya Halmshauri ya Mji wa Geita, kuanzia mwezi
Julai hadi Oktoba 2018, halmashauri hiyo imekusanya jumla ya shilingi
389,699,937.28 kati ya milioni 600,000,000 ilizopanga kukusanya.
Kwa upande wake
Halmashauri ya Wilaya ya Geita kupitia, Afisa Ardhi wake Faraja Kaluwa pamoja
na halmashauri hiyo kupewa malengo ya kukusanya milioni 150 lakini kufikia
desemba 2018 imefanikiwa kukusanya shilingi milioni 12,480,500 tu.
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwataka wakuu wa idara za ardhi katika
halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita kutoa ahadi ya utekelezaji maagizo
aliyoyatoa na hatua gani zichukuliwe kwao iwapo maagizo hayatatekelezwa kwa
wakati.
Maagizo aliyoyatoa Dk
Mabula ni kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya kodi ya ardhi, uingizaji
viwanja na mashamba katika mfumo wa kielektronik, utoaji hati za ardhi pamoja
na utoaji hati za Madai (demand notes) kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi.
Aidha, Dk Mabula
ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinaingiza viwanja na mashamba
kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya kielektronik na kutaka kasi ya utoaji hati
kuongezeka ili kuwawezesha wananchi kiuchumi na wakati huo kuiingizia serikali
mapato kupitia kodi ya ardhi.
Katika hatua nyingine,
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula
amezitaka halmashauri nchini kuhakikisha zinatoa leseni za makazi katika maeneo
yenye nyumba zilizojengwa nje ya urasimishaji na mipango Miji na kueleza kuwa
zoezi hizo linatakiwa kukamilika mwezi machi mwaka huu.
Dk Mabula amezitaka
Halmashauri kuanisha maeneo yote ya nyumba hizo na kupatiwa leseni za makazi
kwa gharama ya shilingi 5000 sambamba na kuziingiza katika kumbukumbu za
halmashauri na kubainisha kuwa leseni hizo ni hatua za kuelekea wamiliki wake
kupatiwa hati.
No comments:
Post a Comment