Tuesday, January 22, 2019

CCM PANGANI YAMTUNUKU TUZO YA SHUKRANI RAIS DKT MAGUFULI KWA UAMUZI WAKE WA KURIDHIA KUTIA SAINI UJENZI WA BARABARA YA TANGA-,PANGANI HADI BAGAMOYO

Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis
Mnegero katikati akimkabidhi tuzo  ya shukrani ya  Rais John
Magufuli ,Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kutokana na
uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu
Abdallah.

Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis
Mnegero akizungumza na waandishi wa habari hatua yao ya kumtunuku tunzo ya shukrani Rais John Magufuli kutokana na uamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa

......................................

CHAMA Cha Mapinduzi wilaya ya Pangani kimemtunuku tunzo ya shukrani Rais John Magufuli kutokana na uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni . 


Akikabidhi tunzo hiyo hapo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya wa Umoja wa wanawake wa chama hicho UWT Taifa Jesca Mbogo wakati akiwa katikaziara ya kukagua shughuli za maendeleo wilayani humo

 
Mwenyekiti CCM wilayani humo Hamis Mnegero alisema kuwa wameamua kutoa tunzo hiyo kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa Rais Magufuli kutoka na kufanikiwa kutekeleza ndoto ya siku nyingi ya kuwa na barabara ya kiwango cha lami wilayani humo.


“Tunajua kuna juhudi kubwa ambazo zilikuwa zimechukuliwa na marais
waliotangulia lakini ndoto hizo hazikuweza kutimia lakini kwa juhudi
kubwa za Rais wa awamu ya tani tumeona ujenzi huo sasa unakwenda
kufanyika”alisema Mnegero.


Alisema kuwa barabara hiyo ilikuwa ni kilio cha muda mrefu kwa
wananchi wa wilaya hivyo anaamini kwa kuanza kwa ujenzi huo kutaweza kufufua matumaini mapya kwa wilaya hiyo.


Kwa upande wake Naibu Katibu mbogo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inajitahidi kuboresha mazingira bora katika sekta mbalimbali ili
kuhakikisha kila mtanzania anapata fursa ya kupata maendeleo na unafuu wa maisha.


“Kama mnavyoona utekelezaji wa sera ya elimu bure pamoja na
uboreshwaji wa huduma za afya hii yote ni kuhakikisha mtoto wa
kitanzania anakuwa na afya bora lakini anapata fursa ya elimu
bora”alisema Naibu Katibu huyo. Naibu Katibu Mkuu Mbogo yupo mkoani Tanga kwa ziara ya siku tatu kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali pamoja na kuzungumza na wanachama wa UWT mkoani hapa


No comments:

Post a Comment