Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi wilaya ya Bagamoyo, Abduli Sharifu, ametoa salamu za mwaka mpya 2019
huku akisema kuwa anathamini michango ya watu wa vyama vyote.
Katika salamu zake hizo,
Sharifu amewataka wa CCM na wanachama wa vyama vingine kuishi kwa umoja na
kushirikiana katika mambo mbalimbali ya maendeleo.
Alisema maendeleo hayana
chama hivyo kila mtanzania bila ya kujali chama chake anapaswa kushiri shughuli
za maendeleo katika eneo lake.
Alisema katika uongozi
wake ndani ya CCM wilaya ya Bagamoyo, atahakikisha wana siasa wote wanaishi kwa
amani na utulivu na kuthamini mawazo ya watu wote.
Aliongeza kuwa, kukosolewa
ni miongoni mwa chaangamoto kuona wapi panahitaji marekebisho ili kuboresha
zaidi.
Katika hatua nyingine
Mwenyekiti huyo wa CCM wilaya ya Bagamoyo alisema katika kipindi hiki ambacho
anatimiza mwaka mmoja katika uongozi wake ameweza kusimamia vyema utekelezaji
wa ilani ya uchaguzi pamoja na kusimamia katiba ya CCM.
Alisema miongoni mwa mambo
ambayo ameyafanya katika kipindi cha mwaka mmoja ni pamoja na kujenga mahusiano
mema kati ya chama na serikali na kuamsha ari kwa wanachama wa CCM.
No comments:
Post a Comment