Mbunge
wa jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Humoud Jumaa akiwa na baadhi ya
kamati ya ujenzi Daraja na mafundi katika Kitongoji cha Ruvu kwa dosa, PICHA NA
OMARI MNGINDO.
...............................
Na
Omary Mngindo, Ruvu
WAKULIMA
zaidi ya 30,000 wanaolima ukanda wa Mto Ruvu jirani na Kitongoji cha Ruvu
Kwadosa, Kata ya Mtambani Mlandizi Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, wanataraji
kunufaika na daraja linalojengwa, katika Kitongoji hicho.
Daraja
hilo linalounganisha mashamba ukanda wa Mto Ruvu na Kitongoji hicho, wakazi
kutoka mikoa ya Pwani, Dar es Salaan na Morogoro wanataraji kunufaika na daraja
hilo, ujenzi ulioanza mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mbunge
wa Jimbo hilo Humoud Jumaa, alifika eneo la ujenzi, na kukutana na
viongozi wa Kamati inayosimamia kazi hiyo, chini ya Mwenyekiti wa Kitongoji
Mohamed Matimbwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mjumbe Beatrice Lugongo.
Akizungumza
katika eneo la ujenzi, Jumaa alisema kuwa kukamilika kwake kunataraji kugharimu
shilingi milioni 30, hivyo kuondoa malalamiko ya miaka mongi, wakiwa na adha ya
kupita kutokana na eneo kuwa na mkondo mkubwa wa kupitisha maji.
"Ujenzi
wa daraja hili, unaotaraji kutumia zaidi ya shilingi milioni 30, utasaidia
kuondoa adha kwa wakulima wanaojihusisha na shughuli hiyo ambayo ndio tegemeo
kwa wananchi, si hapa nchini bali duniani kote," alisema Jumaa.
Matimbwa
alisema kwamba kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili utakuwa mkombozi, kwani kwa
miaka mingi wakulima wa ukanda huo wanataabika hususani kipindi cha mvua.
Mjumbe
Beatrice aliwaomba wananchi wajitolee katika kuchangia ujenzi huo, sanjali na
kujitokeza kwenye eneo la mradi ili liweze kukamilika mapema iwezelanavyo.
No comments:
Post a Comment