NA
MWAMVUA MWINYI, PWANI
MATUKIO
ya ajali za barabarani yamepungua mkoani Pwani, kutoka ajali 91 zilizotokea
mwaka 2017 hadi kufikia ajali 62 zilizotokea kipindi cha mwaka 2018 .
Aidha
mwaka 2017 watu waliokufa kutokana na ajali hizo ni 88 ,na mwaka 2018 ni watu
58 .
Akitoa
taarifa ya makosa ya usalama barabarani kimkoa, katika kipindi cha mwaka
uliopita, kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP) Wankyo Nyigesa alisema
waliojeruhiwa ni watu 136 katika kipindi cha mwaka 2017 na mwaka 2018
waliojeruhiwa ni 97 .
“Kupungua
kwa vifo na ajali zitokanazo na matukio ya ajali za barabarani haimaanishi
madereva waendelee kukiuka sheria za usalama barabarani”..La hasha,”nawataka
watii sheria hizo na watumiaji wengine warekebishe na kuvifanyia matengenezo
vyombo vyao vya moto kabla ya kuviweka barabarani “alisema Wankyo.
Wakati
huo huo, alieleza hali ya uhalifu katika kipindi cha 2018 yamepungua
ukilinganisha na mwaka 2017 ambapo matukio 2,327 yaliripitiwa katika vituo
mbalimbali vya polisi wakati 2017 matukio 2,478 yaliripotiwa.
“Kwa
takwimu hizi tumepunguza matukio 151 makubwa kwa mwaka 2018
ikilinganishwa na mwaka 2017 “alieleza Wankyo.
Wankyo
alibainisha, wanaendelea kupambama na mabasi yanayosafiri kupitia barabara
za mkoa wa Pwani kwa kuyakagua na kuona kama yana ubora wa kufanya usafirishaji
wa abiria.
“Kudhibiti
ujazaji ndani ya mabasi, uzidishaji wa nauli kwa abiria kwa kushirikiana na
SUMATRA, malori na kuyafanyia ukaguzi wa kina katika maeneo yao ya maegesho na
yanapopita kwenye barabara zetu “alisisitiza
No comments:
Post a Comment