Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo ametoa wiki tatu kwa
mhandisi Francis Bago anayesimamia ujenzi wa kituo cha Afya cha Mkonze
Wilaya ya Dodoma, kuhakikisha kituo hicho kimekamirika.
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo
leo jijini Dodoma wakati alipokuwa akikagua miradi mikubwa inayotekelezwa na
Serikali ndani ya Jiji la Dodoma, amesema ndani ya wiki tatu ujenzi wa kituo
hicho uwe umekamirika kwani upo nyuma ya wakati.
Amesema huo ni uzembe kuona kituo
hicho hakijakamirika kwani kipo Mjini lakini ujenzi wake haujakamirika na
unasuasua, wakati vituo vilivyopombali ujenzi wake umekamirika na mgao ulitoka
pamoja na wao wapo mwishoni lakini kituo hicho bado sana.
“Nashangaa kuona kituo hiki kipo
Mjini kabisa ujenzi wake haujakamilika, wakati huo huo kuna vituo vimekamilika
na vipo mbali na fulsa na vifaa vya ujenzi vinapatikana kwa umbali mrefu,
kwahiyo huu ni uzembe na naagiza ndani ya wiki tatu ujenzi huu uwe
umekamilika,” amesema.
Serikali ilitoa kiasi cha shilingi
milioni mia nne(400,000,000) kukamilisha ujenzi wa kituo hicho cha Afya, kiasi
ambacho kilipelekwa katika Halmashauri nyingi katika kuhakikisha vituo vya Afya
vinajengwa.
Vile vile amemtaka mhandisi mshauri
wa Jiji la Dodoma kuhakikisha Mradi wa ujenzi wa pakingi ya Magari makubwa
kilichopo Nala kuhakikisha kinakamilika kwa wakati ili kuanza kutumika,
ameagiza kuhakikisha kinajengwa kwa viwango vinavyotakiwa ili kuepuka kutitia
pindi kikianza kutumika.
Waziri Jafo pia ameridhishwa na hatua
ya ujenzi wa Miradi miwili ya Stendi kubwa ya Mabasi na Soko kubwa linalojengwa
eneo la Nanenane na kampuni ya ujenzi ya Mohamedi Bulder, na kusisitiza
usimamizi thabiti ili miradi hiyo iwe kioo ndani ya Jiji la Dodoma.
Pia amewaagiza Mkuu wa Wilaya na
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuanza mapema kupanga namna ya uendeshaji wa
miradi hiyo ili iwe kuleta tija kwa Serikali na kuwa chachu ya maendeleo ndani
ya Jiji la Dodoma.
Waziri Jafo katika ziara hiyo
amekaagua ujenzi wa kituo cha pakingi ya magari makubwa eneo la Nala, ujenzi wa
kituo cha Afya Nkonze na ujenzi wa Stendi kubwa ya Mabasi pamoja na Soko kubwa
la kimataifa vinavyojengwa eneo la Nanenane ndani ya Jiji la Dodoma.
No comments:
Post a Comment